Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Air Jordan 3 yapata sura mpya, baada ya miaka 40

AIR Pict

Muktasari:

  • Mabadiliko hayo yamezua mjadala mkubwa miongoni mwa wapenda viatu na wanamitindo duniani, wengi wakitaka kujua sababu ya chapa hiyo kubadili moja ya miundo yake iliyodumu kwa miongo kadhaa.

NEW YORK, MAREKANI: Toleo jipya la viatu vya Air Jordan 3 limekuja na muundo unaohifadhi utambulisho wa asili wa viatu hivyo, huku likiongeza maboresho ya kisasa yanayovifanya vijitofautishe na matoleo yaliyotangulia.

Mabadiliko hayo yamezua mjadala mkubwa miongoni mwa wapenda viatu na wanamitindo duniani, wengi wakitaka kujua sababu ya chapa hiyo kubadili moja ya miundo yake iliyodumu kwa miongo kadhaa.

AI 01

Kwa nini mabadiliko haya yamevuta hisia?
Ili kuelewa sababu ya mjadala huo, ni muhimu kurejea mwaka 1988, wakati Air Jordan 3 ilipozinduliwa kwa mara ya kwanza.

Viatu hivyo vilibuniwa na mbunifu maarufu Tinker Hatfield, na vikawa vya kwanza katika familia ya Air Jordan kuwa na teknolojia ya Air unit inayoonekana kwenye kisigino, pamoja na kuanzisha nembo maarufu ya Jumpman kwenye ulimi wa kiatu.

Mbali na ubunifu huo, Air Jordan 3 ilijijengea umaarufu kupitia muonekano wake wa kipekee, ukiwemo michoro ya Elephant Print kwenye sehemu ya mbele na kisigino, muundo wa urefu wa kati (mid-cut) uliorahisisha mchezaji kusogeza kifundo cha mguu, pamoja na uwiano kamili wa muundo wake.

AI 02

Kwa karibu miaka 40, kila jozi ya Air Jordan 3 ilikuwa ikitengenezwa kwa muundo unaofanana kikamilifu kati ya kiatu cha kushoto na cha kulia, jambo lililokuwa sehemu ya utambulisho wake na sababu mojawapo ya kuifanya kuwa miongoni mwa miundo maarufu zaidi katika historia ya viatu vya michezo.

Toleo jipya sasa limeamua kuvunja utamaduni huo kwa kuingiza mabadiliko ya kisasa, huku likihifadhi urithi uliolifanya Air Jordan 3 kuwa moja ya viatu vinavyoheshimika zaidi duniani.