Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni fainali ya Ufaransa na Hispania Olimpiki leo

Muktasari:

  • Ufaransa ilifanikiwa kutinga fainali baada ya miaka 40 baada ya kuichapa Misri mabao 3-1 kwenye mchezo wa nusu fainali uliokwenda hadi dakika za nyongeza.

Paris. Ufaransa ikiwa chini ya kocha Thierry Henry leo inainga uwanjani kwenye mchezo wa fainali wa Olimpiki dhidi ya Hispania, kwenye mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa.

Awali mashabiki wa Ufaransa walilalamika baada ya Henry kupewa timu hiyo wakiamini kuwa kutokuwa na uzoefu mkubwa kutaifanya ishindwe kufanya vizuri, lakini matokeo ya hivi karibuni yamewashangaza.

Ufaransa ilifanikiwa kutinga fainali baada ya miaka 40 baada ya kuichapa Misri mabao 3-1 kwenye mchezo wa nusu fainali uliokwenda hadi dakika za nyongeza.

Hispania yenyewe ilifanikiwa kufika fainali baada ya kuifunga Japan mabao 3-0 kwa mabao mawili kutoka Fermin huku lingine likifungwa na Abel Ruiz na kuifanya timu hiyo kuingia fainali.

"Wakati mwingine sumu inaweza kuwa dawa ikitumika vizuri, nafikiri hawa vijana wanaweza kufanya vizuri tofauti na jinsi ambavyo wengine walikuwa wanafikiri naamini tunakwenda uwanjani kutafuta ushindi, tunajua ubora wa Hispania na imekuwa ikifanya vizuri kila mwaka, lakini nasi tumetengeneza ubora wetu ambao tutakwenda kuutumia," alisema Henry.

Ufaransa ambayo iliwaongeza wachezaji wakongwe kwenye kikosi kama Alexandre Lacazette na Michael Olise ambao wameonyesha kiwango cha juu sana kwenye timu hiyo hadi sasa mara ya mwisho kuchukua ubingwa huu ilikuwa mwaka 1984.

Inaonekana kuwa Ufaransa imeshaamini kuwa inaweza kufanya vizuri kwenye mchezo huu ikiwa imeandaa hafla kwa ajili ya wachezaji wake wa zamani waliofanikiwa kutwaa ubingwa wa mwaka 1984. Mara ya mwisho Ufaransa ilifanikiwa kuichapa Hispania kwenye aridhi ya nyumbani kwenye mchezo wa Euro kwa mabao 2-0.

Hata hivyo, Ufaransa haitegemei mteremko kwenye mchezo huo kutokana na ubora ambao Hispania imeutengeneza kwa miaka ya hivi karibuni wakiwa pia ndiyo mabingwa wa Kombe la Euro na wachezaji.

Morocco ilimaliza nafasi ya tatu baada ya kuichapa Misri mabao 6-0 na kutwaa medali ya shaba, sasa zimebaki medali ya dhahabu kwa bingwa na silver kwa timu itakayoshika nafasi ya pili leo.