Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta atoa matumaini kuhusu jeraha la Raya

Muktasari:

  • Raya alilazimika kutoka uwanjani dakika ya 70 wakati Arsenal ikitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Newcastle United, Jumamosi iliyopita, kwenye Uwanja wa St James' Park.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amewapa matumaini mashabiki wa timu hiyo baada ya kueleza kuwa jeraha la bega alilopata kipa namba moja, David Raya, huenda lisiwe kubwa kama ilivyodhaniwa awali.

Raya alilazimika kutoka uwanjani dakika ya 70 wakati Arsenal ikitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Newcastle United, Jumamosi iliyopita, kwenye Uwanja wa St James' Park.

Kipa huyo aliumia bega la kushoto baada ya kugongana na mshambuliaji wa Newcastle, William Osula, huku akionekana kupata maumivu makali alipokuwa akiondolewa uwanjani.

Hata hivyo, Arteta amesema vipimo vya awali vimeonyesha hali inayotia moyo na hakuna haja ya kufanyiwa upasuaji, jambo ambalo lingemuweka nje ya uwanja kwa miezi kadhaa.

"Kwa sasa hayuko tayari kucheza kesho, lakini jeraha halionekani kuwa kubwa sana. Tunahitaji kufanya vipimo zaidi, lakini matokeo ya awali yanatia moyo," alisema Arteta.

Aliongeza: "Mwanzoni tulihofia jambo baya zaidi kwa sababu alikuwa na maumivu makali kiasi cha kushindwa kuvumilia. Lakini vipimo vya kwanza vimeonyesha hali nzuri zaidi ya tulivyotarajia."

Kutokana na hali hiyo, Kepa Arrizabalaga anatarajiwa kupewa nafasi ya kulinda lango la Arsenal katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, Arteta hajaondoa uwezekano wa Raya kurejea katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester City Jumapili, akisema vipimo zaidi ndivyo vitakavyoamua hatma yake.

Nyota huyo wa zamani wa Arsenal, Ian Wright, amesema kukosekana kwa Raya kutakuwa pigo kubwa kwa timu hiyo kutokana na mchango wake katika uimara wa safu ya ulinzi.

"Ni pigo kubwa sana. Wachezaji kama Raya, Declan Rice na Gabriel ni vigumu kuwapata mbadala wao," alisema Wright.

Wakati hu huo, kiungo Bruno Guimaraes amesema Arteta ni kocha anayezingatia kwa kiwango kikubwa mambo madogo madogo yanayoweza kumfanya mchezaji afike kiwango kingine.

Guimaraes amesema amekuwa akijifunza mengi kutoka kwa kocha huyo, hasa namna ya kudhibiti mpira na kufanya maamuzi sahihi uwanjani.

"Arteta ni wa kipekee. Anazingatia sana mambo madogo madogo ambayo sijawahi kufundishwa kabla. Anaweza kutumia muda mwingi kukuelekeza namna ya kufanya jambo fulani," alisema Guimaraes.