Zungu ataja sababu ya kukaa benchi KVZ
Muktasari:
- Msimu wa 2025-2026 kipa huyo alimaliza msimu akiwa na cleansheet nane hivyo amesema hanamatumaini na kuzifikisha hizo kwa sababu ya kuanza vibaya msimu huu.
KIPA wa KVZ, Idrissa Mguya 'Zungu amesema licha ya kukosa namba kwenye kikosi hicho bado anaamini ana uwezo wa kucheza katika ligi yoyote kwa kiwango chake.
Amesema kutokana KVZ kuwa na makipa wazoefu na wenye uwezo mkubwa kwenye ligi hiyo pengine ndiyo sababu inayofanya kocha wa timu kumuweka benchi.
Kati ya mechi nane ambazo imecheza timu hiyo, Zungu amecheza mechi moja pekee dhidi ya JKU iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.
"Timu ina makipa wengi wazuri wanaofanya nikae benchi mechi nyingi kwa kuwa makipa waliopo wanazoefu kwenye ligi hiyo," amesema
Mbali na hilo, Zungu amesema hapendezwi kukaa benchi kwa sababu kiwango chake kinashuka hivyo anatamani Kocha wa timu hiyo kumuamini na kumpa nafasi.
Kipa huyo, amesema wakati akiwa Fufuni alikuwa na uhakika wa namba zaidi ikilinganishwa na KVZ na tangu kujiunga na timu hiyo amecheza mechi mbili tu dhidi ya Tusker waliyofungwa 2-0 na JKU iliyomalizika kwa sare 1-1.
Msimu wa 2025-2026 kipa huyo alimaliza msimu akiwa na cleansheet nane hivyo amesema hanamatumaini na kuzifikisha hizo kwa sababu ya kuanza vibaya msimu huu.
Pia, amesema anaamini mashabiki wa timu hiyo wana imani kubwa na yeye na ipo siku atawaonesha wanachokitamani kukiona kutoka kwao.