Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zilizopanda daraja Ligi Kuu Zanzibar hali tete

ZILIZOPANDA Pict

Muktasari:

  • Kati ya timu hizo, mbili zinakabiliwa na hatari kubwa ya kushuka daraja endapo zitashindwa kuboresha matokeo katika michezo inayofuata. Timu hizo ni Black Sailors inayoshika nafasi ya 14 na Mwenge SC iliyopo nafasi ya 15.

TIMU nne zilizopanda daraja na kushiriki Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) msimu wa 2026-2027, Black Sailors, Wembe SC, Raskazone FC na Mwenge SC, zimeendelea kukutana na wakati mgumu katika michezo ya mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.

Kati ya timu hizo, mbili zinakabiliwa na hatari kubwa ya kushuka daraja endapo zitashindwa kuboresha matokeo katika michezo inayofuata. Timu hizo ni Black Sailors inayoshika nafasi ya 14 na Mwenge SC iliyopo nafasi ya 15.

Mwenge SC ndiyo inayokabiliwa zaidi na presha hiyo baada ya kushinda mchezo mmoja pekee kati ya 14 iliyocheza, kutoka sare mara tatu na kupoteza michezo 10.

Matokeo hayo yameifanya timu hiyo kukusanya pointi sita pekee, ikiwa imefunga mabao manane na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 23. Hali hiyo ilisababisha mabadiliko ya benchi la ufundi, lakini hadi sasa bado haijaonyesha matokeo yaliyotarajiwa.

Kwa upande wa Black Sailors, imeendelea kuwa kwenye mazingira magumu baada ya kukusanya pointi 10 katika mechi 12. Timu hiyo imeshinda mbili, sare nne na kupoteza sita, hali inayoifanya kuwa ndani ya eneo la kushuka daraja kabla ya mchezo wa jana.

Wembe SC, ambayo pia ilifanya mabadiliko ya kocha kutokana na matokeo yasiyoridhisha, ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza michezo 13. Timu hiyo imeshinda mara tatu, sare tano na kupoteza mechi nne.

Raskazone FC inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 14, baada ya kushinda mechi nne, sare mbili na kupoteza sita.

Wakati timu hizo zikihangaika kujinasua katika hatari ya kushuka daraja na mwisho wa msimu timu nne zinazoshika nafasi ya 12 hadi 16 huwa zinashuka, Zimamoto FC inaendelea kuongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 31, ikifuatiwa na Polisi SC yenye pointi 28 na JKU yenye 26. Bingwa mtetezi KVZ FC, inashika nafasi ya sita kwa pointi 21.