Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ZFF yawageukia wasimamizi wa mechi

Muktasari:

  • Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ZFF, Kibabu Haji Hassan, wakati akizungumza na wasimamizi hao katika semina maalumu iliyofanyika Mwanakwerekwe kisiwani Unguja.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), limewataka wasimamizi wa mchezo kufuata sheria 17 za mpira wa miguu kwa lengo la kufanyakazi kwa ueledi na uaminifu.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ZFF, Kibabu Haji Hassan, wakati akizungumza na wasimamizi hao katika semina maalumu iliyofanyika Mwanakwerekwe kisiwani Unguja.

Mwenyekiti huyo, alisema mafunzo hayo yanalenga kuwakumbusha majukumu yao na kuwaongezea maarifa, ujasiri na uaminifu katika kazi yao.

Hivyo, ametoa rai kwa wasimamizi hao kuyatumia vyema waliyoyapata kwenye mafunzo hayo kwa kuleta mabadiliko ili kukuza soka Zanzibar.

“Tumetoa mafunzo haya kwa ajili ya kusimamia majukumu yenu kwa uaminifu na kuacha kufanyakazi kimazoea kwani tunahitaji kukuza Soka la Zanzibar,” alisema.

Alisema, mafunzo hayo yanakusudia kuwaongezea maarifa na uelewa katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia taratibu na kanuni zilizowekwa.

Aidha, Kibabu alisema mafunzo hayo yanawajengea washiriki ujasiri na kuimarisha uaminifu katika kazi zao, ili waweze kutekeleza majukumu kwa weledi, haki na uadilifu.

Aliongeza kuwa, ujuzi na maadili hayo ni muhimu katika kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa maslahi ya taasisi na jamii kwa ujumla.

Pia, Mwenyekiti huyo, alisema ZFF inahitaji kuona mabadiliko hususani ya uandaaji wa taarifa zinazoendana na uhalisia wa mchezo husika chini ya sheria na kanuni ya mashindano.