Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ZBLP yataja sababu kuongeza viwanja

Muktasari:

  • Ongezeko hilo linafanya sasa Ligi Kuu Zanzibar kuchezwa kwenye viwanja sita kutoka vitatu vya awali ambavyo vilikuwa ni Gombani kisiwani Pemba, Mao A na Mao B kisiwani Unguja.

BODI ya Ligi Zanzibar (ZBL), imetaja sababu ya kuongeza viwanja vitatu ambavyo ni Kinyikani ulioko Pemba, Pangatupu na Kitogani vya Unguja ambavyo vitakatumika kwa mechi za Ligi Kuu Zanzibar msimu wa 2026-2026.

Ongezeko hilo linafanya sasa Ligi Kuu Zanzibar kuchezwa kwenye viwanja sita kutoka vitatu vya awali ambavyo vilikuwa ni Gombani kisiwani Pemba, Mao A na Mao B kisiwani Unguja.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Zanzibar, Issa Kassim Ali, alisema kwa muda mrefu mechi za ligi zimekuwa zikichezwa mjini pekee na kuwafanya mashabiki wa nje ya mji kukosa fursa hiyo.

Alisema, baada ya kugunguda kwamba mashabiki wa mpira wa miguu hawapo mjini pekee, ndiyo sababu msimu huu mechi zimepeleka katika viwanja hivyo vilivyopo nje ya mji.

“Ligi ya Zanzibar itachezwa katika viwanja sita msimu huu ambavyo ni Gombani, Kinyikani, Pangatupu, Kitogani, Mao A na Mao B, tunahitaji kuwafikia wapenzi wa mpira waliopo vijiji,” alisema.

Aliongeza kuwa, pia Serikali inaboresha miundombinu ya viwanja vya michezp ili kupanua wigo wa ligi hiyo kuchezwa katika maeneo tofauti.

Alisema haitapendeza kuona ligi inachezwa uwanja mmoja tu ilihali vingine vipo na vimejengwa kwa lengo la kutumiwa na wananchi kukuza vipaji vyao.

Alifafanua kuwa, pia uwepo wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027 ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji kwa kushirikiana na Kenya na Uganda, ni sababu nyigine inayofanya kuongezwa kwa viwanja hivyo ili kuifanya ligi kumalizika mapema kupisha maandalizi ya mwisho ya fainali hizo.

Alisema ligi zote zinapaswa kumalizika kwa wakati kupisha mashindano hayo, hivyo wasipoongeza viwanja itawawia vigumu kukimbizana na muda.