Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yassin Mustapha kwenye mwawindo ya Kagera Sugar

Muktasari:

  • Beki huyo aliachana na Coastal Union, Agosti 15, 2026, baada ya kuichezea timu hiyo kwa miezi sita tu tangu alipojiunga nayo Januari 29, 2026, akitokea TRA United, huku akicheza pia Polisi Tanzania, Stand United, Mwadui FC na Mtibwa Sugar.

Aliyekuwa beki wa kushoto wa Yanga, Yassin Mustapha yuko katika hatua za mwisho za kujiunga na kikosi cha Kagera Sugar, baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu bila ya timu yoyote, tangu alipoachana na Coastal Union, Agosti 15, 2026.

Beki huyo aliachana na Coastal Union, Agosti 15, 2026, baada ya kuichezea timu hiyo kwa miezi sita tu tangu alipojiunga nayo Januari 29, 2026, akitokea TRA United, huku akicheza pia Polisi Tanzania, Stand United, Mwadui FC na Mtibwa Sugar.

Baada ya kukaa nje ya uwanja tangu, Agosti 15, 2026, bila ya timu yoyote, beki huyo kwa sasa yupo hatua za mwishoni za kujiunga na Kagera Sugar katika dirisha dogo la Januari 2027, ikiwa ni pendekezo pia la Kocha Mkuu, Mrundi Cedric Kaze.

Taarifa kutoka Kagera Sugar, zinadai mchezaji huyo ni pendekezo la Kaze kwa ajili ya kuongeza nguvu na ushindani wa eneo la beki ya kushoto, ambalo mara nyingi amekuwa akitumika, David Charles Luhende katika mechi mbalimbali za kikosi hicho.

Nyota huyo amekamilisha baadhi ya taratibu zote na kinachosubiriwa kwa sasa ni dirisha dogo la usajili la Januari 2027, lifunguliwe ili aanze kukichezea kikosi hicho, ambacho amesaini mkataba wa miezi sita hadi mwisho wa msimu wa 2026-2027.

Beki huyo alikuwa kwenye mazungumzo na baadhi ya timu mbalimbali zikiwemo Mbeya City na Fountain Gate, ingawa amefikia makubaliano ya kutua Kagera Sugar, ambayo muda wowote kuanzia sasa atajiunga nayo ili kuendelea na programu za mazoezi.