Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mido aziingiza vitani Simba, Yanga

Muktasari:

  • Kiungo huyo aliyejiunga na Dodoma Jiji, Januari 12, 2026, akitokea Coastal Union, mkataba wake wa mwaka mmoja na kikosi hicho cha ‘Walima Zabibu’, unafikia tamati Januari 2027, huku vita ya kuiwinda saini yake ikianza mapema kwa vigogo hao.

WAKATI usajili wa dirisha dogo kwa wachezaji wa Ligi Kuu na mashindano mengine ya ndani ukitarajiwa kufunguliwa Januari 2027, Yanga na Singida Black Stars ziko vitani kuiwania saini ya kiungo mshambuliaji wa Dodoma Jiji, Khleffin Hamdoun.

Kiungo huyo aliyejiunga na Dodoma Jiji, Januari 12, 2026, akitokea Coastal Union, mkataba wake wa mwaka mmoja na kikosi hicho cha ‘Walima Zabibu’, unafikia tamati Januari 2027, huku vita ya kuiwinda saini yake ikianza mapema kwa vigogo hao.

Taarifa ambazo Mwanaspoti imezipata, zinadai miongoni mwa timu zinazomfuatilia kwa ukaribu kiungo huyo mshambuliaji ni Yanga na Singida Black Stars, ambazo zimevutiwa na kipaji chake tangu kuanza msimu wa 2026-2027, akiwa na Dodoma Jiji.

Nyota huyo inadaiwa anafanya mazungumzo na wawakilishi wa timu hizo mbili ambazo zimeonyesha nia ya kumuhitaji katika dirisha dogo la Januari 2027, licha ya uongozi wa Dodoma Jiji kuhitaji kumuongezea mkataba mpya wa mwaka mmoja zaidi.

Chanzo kutoka Singida kimeliambia Mwanaspoti, kiungo huyo wanamfuatilia kwa ukaribu ili kupata saini yake katika dirisha dogo la Januari 2027, japo, wamepata taarifa Yanga imeingilia vita hiyo jambo linaloongeza ushindani kati ya pande hizo.

“Ni kweli Singida inafanya mazungumzo na mchezaji huyo lakini hakuna muafaka uliofikiwa hadi sasa, kwa sababu Yanga pia ni timu inayomfuatilia kwa ukaribu, tunaendelea kufuatilia hadi mwisho hali yake itakavyokuwa,” kilisema chanzo hicho.

Kiungo huyo aliyewahi kuichezea Azam FC aliyojiunga nayo Januari 8, 2020, akitokea Mlandege FC ya visiwani, Zanzibar, alijiunga na Dodoma Jiji kwa mkataba wa mwaka mmoja, baada ya kuachana na kikosi cha Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’.

Nyota huyo alijiunga na Coastal Union, Septemba 8, 2025, akitokea Muscat SC ya Oman kwa mkataba wa mwaka mmoja, ingawa, aliutumikia kwa miezi sita tu, kisha kujiunga rasmi na Dodoma Jiji Januari 12, 2026, ambayo huenda akaachana nayo tena.