Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yas, Mixx zaunga mkono Lake Victoria Marathon

VID Pict

Muktasari:

  • Udhamini huo ni sehemu ya mchango wa kampuni hizo katika kuimarisha ustawi wa jamii, ambapo mbio za mwaka huu zimetumika kuhamasisha ukusanyaji wa michango kwa ajili ya watoto njiti, kuhimiza wananchi kufanya mazoezi ya mwili na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ya Ziwa Victoria.

KAMPUNI za Yas na Mixx zimeendelea kuunga mkono juhudi za kuboresha huduma za afya kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti), kupitia udhamini wa msimu wa sita wa mashindano ya mbio za Lake Victoria Marathon yaliyofanyika jijini Mwanza.

Udhamini huo ni sehemu ya mchango wa kampuni hizo katika kuimarisha ustawi wa jamii, ambapo mbio za mwaka huu zimetumika kuhamasisha ukusanyaji wa michango kwa ajili ya watoto njiti, kuhimiza wananchi kufanya mazoezi ya mwili na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ya Ziwa Victoria.

Akizungumza katika hafla ya kufunga mbio hizo, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe. Amiri Mkalipa, alisema Lake Victoria Marathon ni mfano wa namna michezo inavyoweza kuwaunganisha wadau mbalimbali na kuchochea ushiriki wa jamii katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

“Mbio hizi zimetupa nafasi ya kufanya mazoezi na kuhamasishana kuhusu afya, huku tukiwakumbuka watoto njiti wanaohitaji huduma maalumu. Nawapongeza waandaaji, wadhamini Yas na Mixx pamoja na wadau wengine kwa kuunga mkono jitihada hizi,” alisema Mkalipa.

Amesisitiza umuhimu wa wananchi kuendeleza utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara na kushiriki kikamilifu katika kulinda Ziwa Victoria, akieleza kuwa rasilimali hiyo ina mchango mkubwa katika maisha ya wakazi wa mikoa inayolizunguka.

“Wakazi wengi wanategemea Ziwa Victoria kwa chakula, ajira na biashara. Kila mmoja ana wajibu wa kulitunza ili liendelee kutunufaisha sisi na vizazi vijavyo,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Yas, Kanda ya Ziwa Magharibi, Daniel Mainoya, amesema kampuni za Yas na Mixx zimeamua kuunga mkono Lake Victoria Marathon kwa kutambua nafasi ya michezo katika kuhamasisha mshikamano, afya na maendeleo ya jamii.

“Nawashukuru waandaaji kwa kutumia mbio hizi kukusanya michango kwa ajili ya watoto njiti. Iwe umekimbia kwa ajili ya ushindani, kuboresha afya au kufurahi na wapendwa wako, ushiriki wako una umuhimu mkubwa,” alisema Mainoya.

Ameongeza kuwa udhamini huo pia unaakisi dhamira ya kampuni hizo ya kushirikiana na wadau katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kulinda rasilimali muhimu zinazotegemewa na wananchi, hususan katika Kanda ya Ziwa.

Naye Mratibu wa Lake Victoria Marathon, Hilda Viggo, amesema ushirikiano wa Yas, Mixx na wadau wengine umechangia kufanikisha msimu wa sita wa mashindano hayo, ambayo yanalenga kuunganisha michezo na shughuli za maendeleo ya kijamii.

“Tunawashukuru Yas na Mixx, wadhamini wengine na washiriki wote kwa kuwa sehemu ya msimu huu wa sita. Lengo letu limekuwa ni kutumia mbio hizi kuhamasisha mazoezi, lakini pia kuunga mkono huduma za kijamii. Kwa mwaka huu, sehemu ya mapato itaelekezwa kwa watoto njiti na utunzaji wa mazingira ya Ziwa Victoria,” alisema Viggo.

Kupitia udhamini huo, Yas na Mixx zimeendelea kuonesha nafasi ya sekta binafsi katika kuunga mkono matukio yanayochochea afya, mshikamano na ustawi wa jamii, huku Lake Victoria Marathon ikiendelea kuwa jukwaa la kuunganisha michezo na masuala yenye umuhimu kwa wananchi.