Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayanga, Mgunda acha kipigwe

RUANGWA Pict

WAKATI Mbeya City ikishuka uwanjani leo Ijumaa kuwakabili Namungo, Kocha Mkuu wa timu hiyo Salum Mayanga ametamba kuendeleza ubabe Ligi Kuu, huku akiwatahadharisha nyota wake jambo dhidi ya wapinzani hao.

Mbeya City inawakabili wapinzani hao katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Ruangwa mkoani Lindi, ikikumbuka ushindi wa mchezo uliopita dhidi ya Singida Black Stars walipoilaza bao 1-0.

Hata hivyo, mchezo huo unatarajia wa ushindani kutokana na mwenendo wa pande zote, huku Namungo akiwa na takwimu nzuri dhidi ya wapinzani hao kihistoria.

Katika michezo 10 waliyokutana Ligi Kuu, Namungo ameshinda sita, sare mbili na kupoteza miwili, ambapo kwa sasa ‘Wauaji’ hao wa kusini wapo nafasi ya saba kwa pointi 15, huku City wakiwa nafasi 11 kwa pointi 13.

Mayanga amesema mchezo huo ni muhimu sana kwao katika kuendeleza furaha kwa mashabiki na kusaka nafasi nzuri kwenye msimamo, akieleza kuwa hawatawadharau wapinzani kutokana na uwenyeji na ubora wao.

“Tumekuwa na muda mzuri wa maandalizi na matarajio yetu ni kushinda mchezo huo, vijana wapo fiti na tumewatahadharisha kuwa makini na wapinzani ili kufikia malengo” amesema Mayanga.

Kwa upande wake kinara wa mabao katika kikosi cha Namungo, Helbert Lukindo amesema kila mchezo kwao ni hesabu ya pointi tatu, akieleza kuwa baada ya kupoteza mechi dhidi ya Simba, kwa sasa akili zipo kwa City.

“Tuko tayari dhidi ya mchezo huo, tumetoka kupoteza hatutakubali kupoteza tena mechi mbili mfululizo, tunafahamu ugumu lakini umuhimu wa pointi tatu nyumbani” amesema staa huyo.