Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yarudi kambi ya ushindi Dar

Yanga yasaka rekodi mpya

Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga wanaingia kambini Avic Town Kigamboni leo kwa ajili ya kujiandaa na michezo iliyobaki  ya Ligi kuu na Kombe la Shirikisho la Azam.

Wachezaji wa timu hiyo wanatarajia kuwasili leo alasiri kambini ambapo watafanya mazoezi  katika Uwanja wa Avic saa kumi kisha wataendelea na ratiba zao zingine .

Yanga imebakiwa na michezo mitatu ya Ligi kuu na mmoja wa fainali ya Kombe la Shirikisho Azam  ambapo kwenye Ligi mchezo wao wa mwisho nyumbani watawakaribisha timu ya Polisi Tanzania utakaochezwa jumatano jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea jijini Mbeya kuwavaa Mbeya City huku wakitarajiwa kukabidhiwa kombe Lao katika mechi hiyo.