Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakongo watibua sherehe Yanga Day

Muktasari:

  • Les Aigles ikitoka nyuma, imepata ushindi huo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa mabao ya mshambuliaji Tonny Talasi akifunga mawili, ambapo moja kwenye kila kipindi.

Les Aigles du Congo imetibua sherehe za Yanga Day baada ya kuwachapa wenyeji, Yanga SC kwa mabao 2-1.

Les Aigles ikitoka nyuma, imepata ushindi huo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa mabao ya mshambuliaji Tonny Talasi akifunga mawili, ambapo moja kwenye kila kipindi.

Yanga ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao kwa njia ya penalti dakika 27, mfungaji akiwa mshambuliaji Peter Shalulie baada ya kuangushwa na kipa wa Eigles wakati akienda kufunga.

Eigles ikafanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 36 akifunga Talasi akinufaika na makosa ya mabeki wa Yanga waliojichanganya wakati wanataka kuokoa, timu hizo zikaenda mapumziko kwa kufungana bao 1-1.

Kipindi cha pili, Yanga ikafanya mabadiliko ya kikosi kizima lakini kikaruhusu bao la pili kwa makosa yaleyale likifungwa na Talasi na kuifanya timu hiyo kulala kwa mabao 2-1.

Kipigo hicho cha Yanga kinakuja baada ya Simba nayo jana kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Kenya Police ya Kenya, kwenye mchezo wa Tamasha la Simba Day.

Timu hizo mbili zitakutana Agosti12, 2026 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, utakaopigwa Uwanja wa New Amaan Complex kisiwani Unguja.