Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yamponza Kiiza Uganda

Hamis Kiiza

MWANDISHI WETU KOCHA wa timu ya taifa ya Uganda, Bobby Williamson amesema hajamuita kikosini straika wa Yanga yenye ubutu wa mafowadi, Hamis Kiiza kwa sababu alitaka wachezaji wachache wenye kiwango kikubwa. Bosi huyo, ambaye timu yake inacheza na Liberia kesho Jumapili ugenini alisema amesafiri na mastraika watatu ambao ni Geoffrey Massa (Yenicam, Cyprus), Robert Sentongo (St Georges, Ethiopia) na Emmanuel Okwi (Etoile Du Sahel, Tunisia). "Nimeamua kuchukua wachezaji wachache ambao wako kwenye kiwango zaidi kwani tutakuwa ugenini na changamoto ni nyingi,"alisisitiza kocha huyo, ambaye amekuwa akifuatilia kwa karibu rekodi za wachezaji wote wanaocheza nje. Uganda ni ya pili kwenye Kundi J linaloongozwa na Senegal yenye pointi nne. Uganda ina pointi mbili sawa na Angola na Liberia ina pointi moja. Wachezaji wa Simba, Abel Dhaira na Mussa Mudde wameitwa kwenye kikosi hicho huku Kiiza ambaye amekuwa akilalamikiwa hata na kocha wake kwa kukosa mabao mengi akiachwa. Kikosi; Makipa Denis Onyango, Abel Dhaira. Mabeki; Denis Guma, Isaac Isinde, Godfrey Walusimbi, Joseph Ochaya, Henry Kalungi na Andrew Mwesigwa. Viungo; Said Kyeyune, Mussa Mudde, Hassan Wasswa, Boban Zirintusa, Geoffrey ëBabaí Kizito, Moses Oloya na Mike Mutyaba.