Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaipiga bao jingine Simba

MWANDISHI WETU SIMBA inahaha kukikimbiza kivuli cha Yanga kwenye Ligi ya Bara lakini rekodi zinawabeba vijana hao wa Jangwani huku kocha wao, Ernest Brandts akisisitiza kuwa hilo ni bao jingine. Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwa na pointi 42. Imewazidi mabingwa watetezi, Simba wanaohaha nafasi ya tatu kwa pointi 11. Vijana hao wa Jangwani ambao jana Jumatatu walirejea mazoezini jijini Dar es Salaam, wamecheza mechi 18 kama Simba na Azam iliyo nafasi ya pili kwa pointi 36 lakini vinara hao wamefungwa mabao 12 tu ambayo ni machache zaidi, wamepachika mabao 35 ambayo ndiyo mengi zaidi kufungwa kati ya timu zote 14 zinazoshiriki ligi hiyo. Katika mabao, Azam imefungwa 15 na kufunga 31 wakati Simba imefungwa 15 na kufunga 26. Rekodi za Yanga tangu Septemba mwaka jana chini ya kocha Mholanzi, Ernest Brandts ni za aina yake na si Simba wala Azam imeziweza. Rekodi za Yanga chini ya Brandts zinaonyesha kuwa imeshinda asilimia 65 ya mechi zake 20 (pamoja na zile za kirafiki za ndani na nje ya nchi). Katika mechi hizo imeshinda mechi 13 na kupoteza nne huku tatu zilizobaki ilitoka sare. Rekodi hizo tangu mechi ya kwanza ya Brandts ni kama ifuatavyo; Yanga 1-1 Simba SC, Yanga 0-1 Kagera Sugar, Yanga 3-1 Toto African, Yanga 3-2 Ruvu Shooting, Yanga 3-0 Polisi Moro, Yanga 1-0 JKT Oljoro, Yanga 3-0 JKT Mgambo, Yanga 2-0 Azam, Yanga 2-0 Coastal, Yanga 0-1 Tusker (kirafiki), Yanga 1-1 Ariminia Bielefed (kirafiki) na Yanga 0-2 Emmen FC (kirafiki). Nyingine ni Yanga 1-2 Denizlispor FC (kirafiki), Yanga 3-2 Black Leopard (kirafiki), Yanga 2-1 Black Leopard (kirafiki), Yanga 3-1 Prisons, Yanga 1-1 Mtibwa Sugar, Yanga 4-0 African Lyon, Yanga 1-0 Azam na Yanga 1 - 0 Kagera Sugar. Rekodi hizo zinaonyesha Yanga imetoka sare asilimia 15 na kupoteza asilimia 20. Akizungumzia suala hilo, Brandts amesisitiza kuwa anataka kuipa Yanga ubingwa bila kuharibu rekodi yake na kwamba kwa hali ilivyo haoni wa kumtisha kufanya hivyo ingawa anachukua tahadhari kubwa kwa Simba na Azam. "Najivunia kufikia hatua hiyo, kikosi changu kina uwezo na wachezaji wengi wana viwango vinavyoendana. Kuna mambo madogo madogo tu ambayo nayakazania ili timu izidi kuwa sawa hasa suala la ushambuliaji," alisema. "Mara nyingi napenda soka la pasi na timu yangu imeonyesha mabadiliko katika jambo hilo, inacheza soka ninalotaka. Muda unavyoenda mashabiki watarajie mambo mazuri zaidi." Katika hatua nyingine, Brandts amegundua mbinu za kuwafanya mastraika wake Jerry Tegete, Mrundi Didier Kavumbagu, Said Bahanuzi na Khamis Kiiza wawe fiti zaidi kwa kuwajengea mazingira ya kujiamini maradufu.