Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga, Manqoba imeisha hiyoo, awaaga wachezaji

KAAGA Pict

Kikao cha Kamati ya Utendaji ya  Yanga kimefanya uamuzi mgumu wa kubariki kusitishiwa mkataba kwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Manqoba Mngqithi na benchi lake.

Kikao hicho kilichofanyika usiku huu kwa njia ya mtandao, kimetoa uamuzi wa mwisho ambao ni kocha huyo kupewa mkono wa kwaheri ikiwa ni saa chache tangu Yanga ipate sare ya kwanza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ugenini dhidi ya TRA United kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, leo Jumamosi, Oktoba 24, 2026.

Mbali na uamuzi huo kikao hicho kimeitaka sekretarieti ya Yanga kuanza mchakato wa haraka wa kutafuta kocha mpya atakayechukua nafasi ya raia huyo wa Afrika Kusini.

Muda mfupi uliopita uamuzi huo tayari umemfikia kocha Manqoba ambaye katika kikao cha timu hiyo kilichofanyika usiku huu jijini Arusha, amewaaga wachezaji wake akiwatakia kila la kheri.

Wakati wowote kutoka sasa Yanga itatoa taarifa kamili juu ya uamuzi huo mgumu unaokuja baada ya timu hiyo kuangusha pointi tano katika mechi nane ilizocheza mpaka sasa