Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga, Libolo vita ya kufa mtu

NA MWANDISHI WETU KISHABIKI mitaani Yanga inaifurahia Recreativo Libolo ya Angola kwa mambo mawili; kumwondoa mtani wake ambaye ni Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika tena kwa idadi ya mabao 5-0. Yanga wanafurahia kishabiki na kubeba mabango uwanjani kwa vile Simba iliwachapa idadi hiyo ya mabao kwenye ligi msimu uliopita hivyo ni kama Waangola hao wamewalipizia kisasi ingawa si uzalendo. Lakini Yanga watanywea na kufuta urafiki huo wa bandia muda si mrefu baada ya Libolo kupenyeza mkono wao wakiahidi kumsajili winga anayeichezea Simba kwa mkopo, Mrisho Ngassa ifikapo Juni mwaka huu. Ngassa amepelekwa na Azam kwa Simba kwa mkopo na mkataba wake unamalizika Mei huku Yanga ikielezwa tayari imeshafanya makubaliano na mchezaji huyo kwa ajili ya msimu ujao na amewaambia vigogo wa usajili wa Jangwani kwamba wasiwe na wasiwasi atavaa uzi wao. Libolo walizungumza na aliyekuwa Mwenyekiti wa Usajili wa Simba, Zacharia Hanspope mjini Luanda, Angola wiki hii wakamwambia kuwa wanakuja nchini mwezi Juni na kwamba Ngassa asiende popote watakuja kumsainisha pamoja na beki Juma Nyosso. Hanspope alisema: "Wamesema watawasiliana nasi katika dirisha la mwezi Juni na watakuja kukamilisha taratibu za Ngassa na Nyosso, wakataka wasiende pengine, hawawezi kuwachukua sasa hivi kwavile bado kuna muda mrefu na hiki si kipindi cha usajili." "Wameweka wazi pia kwamba wanaendelea kutafuta wachezaji wengine wakipata wachezaji wazuri zaidi ya Ngassa na Nyosso wanaweza kuachana nao,îalisema Hanspope ambaye amejiuzulu wadhifa wake wa usajili Simba huku akishinikiza na viongozi wengine nao wabwage manyanga wakamchomolea ingawa ana sapoti kubwa ya Kundi la Friends of Simba. Simba wamekuwa wakisisitiza kuwa Ngassa amesaini nao mkataba wa mwaka mmoja ingawa kikanuni haikubaliki kwa vile bado alikuwa hajamaliza mkopo wake, lakini Yanga nao vigogo wake wa usajili wamemuonyesha Ngassa mkataba wa muda wa miaka miwili na wana imani kwamba msimu ukiisha ni mali yao na tayari wamempa kitita cha Sh 20 milioni cha kushika uchumba. Libolo wameahidi kumlipa Ngassa dola 15,000 kwa mwezi (Sh 24 milioni) huku Nyosso akikadiriwa dola 10,000 (Sh 16 milioni) lakini bado hawajataja madau ya kuwanunua mpaka mwezi Mei. Yanga italazimika kujipinda kuuongeza dau ili kumbakiza Ngassa ambaye takwimu za fedha zinamshawishi kusaini Libolo, ingawa amekuwa mgumu kucheza nje ya Tanzania. Ngassa amewaambia viongozi wa Simba kuwa atatoa hatima yake ya kujiunga au kutojiunga na Libolo mara akishatuliza akili yake jijini Dar es Salaam na jana Ijumaa alikuwa hapatika hewani. Nyosso kwa upande wake alisema; "Mimi ni askari na mpiganaji. Niko tayari kujiunga na Libolo muda wowote ule wakinihitaji ilimradi tukikubaliana. Nyosso anaweza kwenda Libolo bure baada ya mkataba wake kumalizika mwisho mwa msimu huu wa ligi ambayo Simba inachechemea.