Wydad, Kaizer hapatoshi.
WAKATI wakibakiwa na mechi moja tu kutinga fainali baada ya ushindi wa kwanza dhidi ya Wydad, Kaizer Chiefs watakuwa na shughuli pevu ya kulinda ushindi wao wa kwanza baada ya kushinda goli 1-0 wakiwa ugenini. Mwanaspoti inakuleta makala juu ya timu hizi mbili kuelekea mchezo wa kesho.
TAKWIMU
Wydad imecheza michezo 10, ikishinda michezo sita, ikitoka sare michezo 2, ikipoteza michezo miwili, magoli ya kufunga 14 , na magoli ya kufungwa matatu.
Kwenye hatua ya awali Wydad iliifunga timu ya Stade Malien (Mali) kwa ujumla wa magoli 3-1.
Walikuwa kwenye kundi C pamoja na Kaizer Chiefs,(Afrika Kusini), Horoya (Guinea) na Petro de Luanda (Angola) na Wydad wakimaliza kinara wa kundi wakiwa na pointi 13 wakishinda michezo minne, wakitoa sare mechi moja na kupoteza mechi moja.
Kwenye hatua ya robo fainali Wydad waliifunga timu ya MC Alger ya Algeria kwa jumla ya mabao 2-1.
Kaizer Chiefs imecheza michezo 12, ikishinda michezo mitano, ikitoka sare michezo mitano, na kupoteza michezo miwili huku ikifunga magoli 11 na kuruhusu magoli 9.
Kaizer Chiefs ilianza kwenye hatua za awali ambapo iliifunga timu ya PWD Bamenda ya Cameroon bao 1-0, huku kwenye hatua ya kwanza Kaizer Chiefs iliifunga timu ya Primeiro de Agosto ya Angola kwa jumla ya goli 1-0.
Walikuwa kwenye kundi C pamoja na Wydad, (Morocco), Horoya (Guinea) na Petro de Luanda (Angola) na Kaizer Chiefs wakimaliza kundi wakiwa nafasi ya pili wakiwa na pointi 9, baada ya kushinda michezo miwili, wakitoka sare michezo mitatu na kupoteza mchezo mmoja.
Hatua ya robo fainali Kaizer Chiefs iliifunga timu ya Simba (Tanzania) kwa jumla ya magoli 4-3.
Wydad ni mabingwa mara mbili kwenye michuano hii ya kombe la klabu bingwa Afrika huku mara ya mwisho kuchukua ni Mwaka 2017.
Kaizer Chiefs inacheza hatua hii ya nusu fainali kwenye Ligi ya mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza katika historia ya timu hiyo.
Timu hizi zimekutana mara mbili kwenye ligi ya mabingwa Afrika huku Wydad wakishinda mechi moja na Kaizer Chiefs wakishinda mechi moja, Wydad wakifunga magoli manne na Kaizer Chiefs wakifunga goli moja.