Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Pembe aongeza morali Zanzibar Spice Boys

WAZIRI Pict

Muktasari:

  • Katika hafla hiyo, Waziri huyo, amekabidhi Sh500,000 kwa kila mchezaji wa timu hiyo kuwasaidia katika safari yao huku akiwaombea safari njema yenye mafanikio na kuwataka kuitangaza vyema Zanzibar.

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Riziki Pembe Juma, amewapongeza wazazi wa wachezaji  chipukizi wa timu ya Zanzibar Spice Boys kwa kuwaunga mkono kushiriki fursa ya mashindano ya PQ Cup Brazil 2026.

Waziri huyo ameyasema hayo Septemba 30, 2026 katika hafla ya kuwaaga vijana hao iliyofanyika Ukumbi wa Hoteli ya New Amaan Complex, Unguja.

Amepongeza hatua ya wazazi kujitokeza kuwaunga mkono watoto wao kwani safari hiyo itawapa vijana uzoefu, kujiamini na kuwajengea uwezo wa kushiriki michuano ya kimataifa.

“Twendeni tukachangamkie fursa na  kuzitafuta nyingine ili tutakaporejea tuwe na kitu cha kuleta ushirikiano na kufungua milango yetu,” amesema.

Pia amewataka wadau mbalimbali kujitokeza kuwaunga mkono vijana hao waliopata fursa ya kuiwakilisha Zanzibar na Tanzania nchini Brazil, ili kuwapa moyo na ari ya kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Katika hafla hiyo, Waziri huyo, amekabidhi Sh500,000 kwa kila mchezaji wa timu hiyo kuwasaidia katika safari yao huku akiwaombea safari njema yenye mafanikio na kuwataka kuitangaza vyema Zanzibar.