Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili waruhusiwa kurudi Yanga

Muktasari:

  • Mwanaspoti iliandika safari ya mastaa hao wiki iliyopita kwa ajili ya vipimo, huku kikosi kizima kikielekea nchini Botswana kucheza mechi ugenini dhidi ya Gaborone United.

WACHEZAJI wa Yanga, Clement Mzize na Dickson Job, wamepewa ruhusa na madaktari waliokuwa wakiwasimamia nchini Afrika Kusini kuanza mazoezi pamoja na kikosi hicho, hatua inayowafungulia mlango wa kurejea kwenye ushindani baada ya kipindi cha kuwa nje.

Mwanaspoti iliandika safari ya mastaa hao wiki iliyopita kwa ajili ya vipimo, huku kikosi kizima kikielekea nchini Botswana kucheza mechi ugenini dhidi ya Gaborone United.

Mzize na Job wamerejea nchini usiku wa kuamkia leo wakitokea Afrika Kusini, walikokwenda kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na kupata tathmini ya hali zao kabla ya kuendelea na programu ya mazoezi.

Taarifa za ndani zililiambia Mwanaspoti kuwa baada ya majibu ya vipimo kuonyesha wanaweza kuanza kuongeza mzigo wa mazoezi, madaktari hao wamewaruhusu kuingia kwenye mazoezi ya pamoja ya kikosi, badala ya kuendelea na programu maalumu za kurejea uwanjani kama ilivyokuwa awali.

“Kurejea kwao kunakuja wakati muhimu kwani uwepo wa wachezaji hao unaongeza chaguo na upana wa kikosi, huku benchi la ufundi likipata nafasi ya kuanza kuwarudisha taratibu kwenye mfumo wa ushindani.

“Kuanza mazoezi hakumaanishi kwamba wawili hao wataanza moja kwa moja kwenye mechi. Wanahitaji kupewa dakika chache kwa awamu, huku benchi la ufundi likifuatilia namna miili yao inavyokabiliana na mzigo wa mazoezi na ushindani.”

Kocha Manqoba Mngqithi aliwahi kuliambia Mwanaspoti kuwa kurejea kwao kutazalisha ushindani mkubwa wa nafasi ndani ya kikosi, jambo ambalo benchi lake la ufundi linahitaji katika msimu wenye ratiba ndefu ya ligi na mashindano ya kimataifa.

Huku akiweka wazi kuwa wanaweza kuwa sehemu ya kikosi kuelekea mechi ya dabi.

Mzize aliumia goti na baadaye kufanyiwa upasuaji, hali iliyomweka nje ya uwanja kwa muda mrefu. Baada ya kurejea na kuanza kuonekana katika programu za timu, alikumbana tena na tatizo la goti wakati wa maandalizi ya mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Kabylie, Februari 15, 2026.