Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota waliogeuka maadui wa timu zao za zamani

Muktasari:

  • Wakati Ligi Kuu Bara ikiendelea kushika kasi, wapo baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa mwiba mchungu kwa timu walizowahi kucheza mwanzoni, baada ya kuzifunga mabao msimu huu wa 2026-2027, walipokutana kama Mwanaspoti linavyowaeleza kwa kina.

MSIMU wa 2026-2027 wa Ligi Kuu Bara, umeanza kwa kasi ya aina yake kutokana na ushindani unaoendelea kuonyeshwa na timu zote 16, zinazoshiriki, sambamba na wachezaji mbalimbali ambao wamekuwa na mwendelezo mzuri wa viwango vyao hadi sasa.

Wakati Ligi Kuu Bara ikiendelea kushika kasi, wapo baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa mwiba mchungu kwa timu walizowahi kucheza mwanzoni, baada ya kuzifunga mabao msimu huu wa 2026-2027, walipokutana kama Mwanaspoti linavyowaeleza kwa kina.

OBREY CHIRWA (GEITA GOLD)

Mshambuliaji huyu raia wa Zambia anayeichezea kwa sasa Geita Gold, amekuwa katika kiwango bora baada ya kufunga mabao manne ya Ligi Kuu Bara msimu huu, huku kati ya hayo akizifunga timu alizowahi kuzichezea kabla ya kutua kikosini humo.

Nyota huyo aliifunga Kagera Sugar aliyoichezea msimu wa 2025-2026, mabao mawili ya ushindi wa Geita Gold wa mabao 6-2, katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Bukombe unaopatikana mji mdogo wa Ushirombo, Wilaya ya Bukombe, mkoani Geita.

Mechi hiyo ya Agosti 22, 2026, ilishuhudiwa Chirwa akifunga dakika ya 23 kwa penalti na 69, huku mengine yakifungwa na Richardson Ng’ondya dakika ya 10 na 62 na Yusuph Mhilu dakika ya 37 na 45 ambao wote watatu walifunga mawili kila mmoja. Mabao ya Kagera katika mechi hiyo yalifungwa na Hassan Mwaterema dakika ya 40 na Robert Mathias dakika ya 90+1, ikiwa ni kipigo kikubwa kwa kikosi hicho ambacho hadi sasa hakijaonja ladha ya ushindi kwenye mechi zake tano za Ligi Kuu Bara.

Pia, mshambuliaji huyo aliifunga Azam FC aliyowahi kuichezea Novemba 8, 2018, akitokea Nogoom FC ya Misri katika sare ya mabao 2-2, ambapo mechi hiyo iliyokuwa na ushindani ilichezwa, Agosti 28, 2026, kwenye Uwanja wa Bukombe, mkoani Geita.

Katika mechi hiyo, Chirwa alifunga bao kwa penalti dakika ya 45+8 na lingine likifungwa na Martin Kigi dakika ya 90+3, huku ya Azam FC yakifungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ kwa penalti pia dakika ya 45+2 na Himid Mao Mkami dakika ya 90+1. Mshambuliaji huyo, anashikilia rekodi ya mchezaji wa kwanza wa Ligi ya Championship msimu wa 2025-2026, kufunga mabao matatu (Hat-Trick), wakati kikosi hicho cha Kagera Sugar, kilipoifunga Hausung FC ya Njombe mabao 3-1, Desemba 2, 2025.

Msimu wa 2025-2026, unabakia katika kumbukumbu nzuri kwa Chirwa, kwani nyota huyo aliibuka mfungaji bora akiwa na Kagera Sugar aliyoifungia mabao 18, ikiwa ni idadi sawa na ya Maulid Shaban wa Geita Gold ambao msimu huu wanacheza kwa pamoja.

Miongoni mwa kumbukumbu nzuri kwa Chirwa katika soka la Tanzania, ni kuibuka mfungaji bora wa Kombe la Shirikisho la FA, ambapo nyota huyo anakumbukwa msimu wa 2016-2017, alipoibuka kinara baada ya kufunga mabao matano wakati akicheza Yanga.

Nyota huyo aliibuka kidedea msimu huo wa 2016-2017, ikiwa ni msimu wa pili tangu michuano hiyo iliporejea tena kuchezwa, baada ya kutofanyika kwa miaka 13, mfululizo, tangu mara ya mwisho iliposimama ikifahamika kama Kombe la FAT mwaka 2002.

Katika msimu wa 2016-2017, Chirwa alifunga mabao hayo matano ya Kombe la FA na kuibuka kinara wa ufungaji bora, ingawa, nyota huyo alikosa ubingwa huo wa michuano hiyo, baada ya kuchukuliwa na watani zao Simba iliyoifunga Mbao FC mabao 2-1.


CRISPIN NGUSHI (MASHUJAA FC)

Crispin Ngushi ni miongoni mwa washambuliaji waliozifunga timu walizowahi kuchezea, ambapo mshambuliaji huyo aliifungia Mashujaa FC bao moja, katika ushindi wa kikosi hicho wa 1-0, dhidi ya Coastal Union, aliyochezea kwa msimu wa 2023-2024.

Mshambuliaji huyo aliyewahi kuwika na timu mbalimbali ikiwemo Yanga, alifunga bao hilo dakika ya 86 na kuipa Mashujaa FC pointi tatu muhimu, katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini, Tanga, Agosti 15, 2026.

YUSUPH MHILU (GEITA GOLD)

Yusuph Mhilu sio jina geni kwa mashabiki wa soka nchini, baada ya kuzichezea Yanga na Simba kwa nyakati tofauti, ambapo kwa sasa mshambuliaji huyo anacheza msimu huu Geita Gold, aliyojiunga nayo rasmi, Julai 21, 2023, akitokea Kagera Sugar.

Mshambuliaji huyo aliifunga Kagera Sugar aliyowahi kuichezea mabao mawili ya ushindi wa Geita Gold wa mabao 6-2, katika mechi kali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Bukombe unaopatikana mji mdogo wa Ushirombo, Wilaya ya Bukombe, mkoani Geita.


HIJJAH SHAMTE (MASHUJAA FC)

Kiungo huyo alijiunga na Mashujaa FC msimu huu akitokea Mbeya City, ambapo tayari ameifunga timu aliyowahi kuichezea bao moja, licha ya kikosi hicho cha maafande kukutana na kichapo ugenini cha mabao 2-1, mechi iliyopigwa, Agosti 23, 2026.

Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini, Mbeya, Shamte aliyeichezea pia Kagera Sugar, alifunga bao dakika ya 52, huku Mbeya City ikichomoa kupitia Adilly Buha dakika ya 69 kwa mkwaju wa penalti na Oscar Mwajanga dakika ya 79.

ANUARY JABIR (POLISI TZ)

Nyota huyu aliyejiunga na Polisi Tanzania msimu huu akitokea Dodoma Jiji, alikuwa mwiba mkali kwa waajiri wake wa zamani baada ya kufunga bao moja muhimu la kikosi hicho cha maafande katika ushindi wa 1-0, mechi iliyopigwa, Agosti 25, 2026. Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini, Dodoma, Anuary alifunga bao hilo dakika ya 28, huku nyota huyo akiichezea pia Kagera Sugar na kupata nafasi ya kufanya majaribio katika Klabu ya KAA Gent ya Ubelgiji, Aprili 4, 2023.

MUDATHIR SAID (KAGERA SUGAR)

Mshambuliaji huyu kwa sasa anaichezea Kagera Sugar baada ya kuachana na kikosi cha maafande wa Mashujaa FC ya Kigoma, ambapo katika mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya timu hizo, Mudathir Said alifunga bao moja katika kichapo cha mabao 2-1.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, Agosti 27, 2026, Mudathir aliifungia Kagera bao dakika ya 38, huku Mashujaa FC ikifunga mabao yake kupitia Mishamo Michael (64) na Haroun Lyawatwa (72).