Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanariadha Mwanza, Manyara wang'ara mbio za Kanda ya Ziwa

WANARIADHA Pict

Muktasari:

  • Mbio hizo ambazo ni msimu wake wa sita, zimefanyika Jumapili ya Novemba 15, 2026 katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, zikishirikisha wakimbiaji zaidi ya 3,000 kutoka ndani na nje ya nchi.

WANARIADHA kutoka mikoa ya Mwanza, Singida na Manyara wameng'ara katika mbio za Lake Victoria Marathon mwaka 2026.

Mbio hizo ambazo ni msimu wake wa sita, zimefanyika Jumapili ya Novemba 15, 2026 katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, zikishirikisha wakimbiaji zaidi ya 3,000 kutoka ndani na nje ya nchi.

Washiriki wamechuana kwenye mbio za KM 21, KM 10 na KM 5, huku lengo likiwa ni kuchangisha fedha za kusaidia matibabu ya watoto njiti mkoani Mwanza.

Mwanariadha kutoka Mwanza, Robert Makenzi ameshinda KM 21 kwa wanaume, huku Emmanuel Joseph wa Singida akishika nafasi ya pili, na Fidelis Mwakalambo wa Singida akimaliza wa tatu.

Kwa upande wa wanawake, Tunu Raphael wa Mwanza ameibuka mshindi wa kwanza KM 21, huku Neema Sanka wa Manyara akiwa wa pili na Magdalena Neta wa Shinyanga akimaliza wa tatu.

Mbio za KM 10 kwa wanaume, John Joseph wa Singida ameshinda nafasi ya kwanza, Jamal Saidi kutoka Simbu Foundation ya Manyara akiwa wa pili, na Gabriel Weka wa Manyara akimaliza wa tatu.

Aidha, Atwidi Setti wa Manyara ameibuka mshindi wa kwanza KM 10 kwa wanawake, huku Naomi Marja wa Manyara akishika nafasi ya tatu, na Ednesta Iddi wa Singida akishika nafasi ya tatu.

Robert Makenzi aliyeshinda kilomita 21, amesema ushindi wake umechangiwa na mazoezi anayofanya na dhamira ya kuitangaza Mwanza mbele ya wanariadha kutoka mikoa mingine.

"Nafurahia kupata ushindi huu, ni mbio ya nyumbani nimeshiriki kujitangaza. Ninashauri waandaaji waboreshe zawadi kwa washindi ili kuvutiwa watu wengi kwa sababu kwetu hii ni kazi," amesema  Makenzi.

Naye, Tunu Raphael wa Manyara, amesema mbio hizo zimekuwa kivutio kikubwa na zinaendelea kuwavutia watu wengi, hivyo waandaaji wanapaswa kuziboresha kwa kutoa zawadi zinazovutia kuliko ilivyo sasa.

"Siku zote kwenye riadha hakuna uchawi ni mazoezi. Najisikia vizuri kuwa sehemu ya kushiriki kuchangia kuokoa maisha ya watoto njiti," amesema  Tunu.

Mratibu wa Lake Victoria Marathon, Hilda Viggo amesema mwitikio umekuwa mkubwa kwani walitarajia washiriki 3400 na waliofika ni 3200, huku fedha zilizopatikana wakitarajia kwenda kutoa msaada wa matibabu kwa watoto njiti zaidi ya 600 katika kituo cha afya Buzuruga wilayani Ilemela.

"Tatizo la watoto njiti hali bado ni ngumu kwa mfano kwa mwezi huu tu tumeambiwa wamezaliwa watoto 650 njiti pale Buzuruga, lakini na sisi tunajitahidi pale tunapoweza. Tunatoa wito kwa wadau kusaidia watoto hawa wa Kanda ya Ziwa," amesema Hilda.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amiri Mkalipa amesema uwepo wa mbio hizo umeleta mchango chanya kwa mkoa wa Mwanza na kuongeza mzunguko wa fedha na uchumi kwa wananchi.

"Kwa niaba ya serikali tunawashukuru kwa kufanya mbio hizi kwa kiwango kikubwa na kuzifanya ziwe kubwa. Wito wangu kwa wananchi ni kuendelea kushiriki Ili kuimarisha afya na kubadilisha maisha ya watoto njiti," amesema Mkalipa.