Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakenya wang'ara gofu Zanzibar

WAKENYA Pict

Muktasari:

  • Mashindano hayo yaliyofanyika katika uwanja wa gofu wa Sea Cliff Resort & Spa Zanzibar, yalishirikisha zaidi ya wachezaji 80 kutoka Tanzania Bara, Zanzibar, Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, Afrika Kusini na Nigeria.

WACHEZAJI wa gofu kutoka Kenya, Thomas Mwangi na Caroline Muigai wametwaa ubingwa wa jumla kwa wanaume na wanawake mtawalia katika mashindano ya gofu ya CEOs Luxury Retreat 2026 yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC.

Mashindano hayo yaliyofanyika katika uwanja wa gofu wa Sea Cliff Resort & Spa Zanzibar, yalishirikisha zaidi ya wachezaji 80 kutoka Tanzania Bara, Zanzibar, Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, Afrika Kusini na Nigeria.

Mwangi alitwaa ubingwa wa jumla kwa wanaume baada ya kukusanya pointi 40, huku Muigai akiibuka kinara kwa wanawake kwa pointi 41 katika mashindano yaliyochezwa kwa mfumo wa Stableford katika mashimo 18.

Mashindano hayo yaliunganisha ushindani wa gofu na fursa ya viongozi wa biashara kukutana, kubadilishana mawazo na kujenga mahusiano ya kikazi, huku pia yakitoa nafasi ya kuitangaza Zanzibar kama moja ya vivutio vya utalii.

Katika Division A, Patrick O’Rourke alitwaa nafasi ya kwanza, huku Ernest Sengeu akimaliza wa pili kwa pointi 31.

Thagaran Govender alishinda Division B kwa pointi 39, akifuatiwa na Gregory Eayrs aliyepata pointi 38. Katika Division C, Abbas Simkoko alitwaa ushindi kwa pointi 40, akifuatiwa na Joseph Sayi aliyepata pointi 37.

Kwa upande wa wanawake, Salome Gakere alishinda kwa pointi 36, huku Vicky Elias akimaliza nafasi ya pili baada ya kufungana pointi 35 na Maryanne Mugo na kuamua kwa mfumo wa countback.

Vodacom Tanzania ilikuwa mdhamini mkuu wa mashindano hayo yaliyowakutanisha maofisa wakuu watendaji wa kampuni, wanadiplomasia, viongozi wa biashara na wapenzi wa mchezo wa gofu kwa siku ya michezo, mawasiliano na uhusiano wa kibiashara.

Akizungumza wakati wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando, amesema kampuni hiyo inajivunia kuunga mkono mashindano yanayounganisha michezo na jamii ya wafanyabiashara.

“Tunafurahia kuhusishwa na mashindano ya CEOs Luxury Retreat kwa sababu gofu si mchezo pekee, bali ni jukwaa linalowakutanisha watu, mawazo na fursa,” amesema Komando.

Amesema mashindano hayo yanatoa mazingira rafiki kwa viongozi wa biashara kutoka sekta mbalimbali kukutana na kujenga mahusiano ya kikazi.

“Mashindano haya yanawakutanisha viongozi kutoka sekta mbalimbali na kutoa fursa za kujenga mitandao, ushirikiano na kubadilishana mawazo,” amesema.

Kamando pia alihusisha mashindano hayo na juhudi za kukuza utalii Zanzibar, akisema matukio ya kimataifa ya michezo yanaweza kuitangaza Zanzibar kwa wageni ambao wanaweza kurejea kwa ajili ya utalii au shughuli za kibiashara.

“Tunajivunia kushiriki katika kuitangaza Zanzibar kama kituo cha biashara, utalii na michezo. Matukio kama haya yanaongeza thamani si kwa washiriki pekee, bali pia kwa uchumi kwa ujumla,” amesema.

Amesema ushiriki wa Vodacom katika mashindano hayo ni sehemu ya kuunga mkono mipango inayowakutanisha watu na wadau mbalimbali katika jamii.

“Ushirikiano wetu na mashindano haya unaakisi dhamira yetu ya kuunga mkono majukwaa yanayowaunganisha watu na kuleta matokeo yenye manufaa ya kudumu,” amesema Kamando.