Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafanyakazi wa Hoteli ya Oakland’s Afrika Kusini wamlilia Kibonde

Muktasari:

Kibonde alikuwa akitumia hoteli hiyo pamoja na wenzake walipokuwa wakienda Afrika Kusini kwa shughuli za kikazi.

Wafanyakazi wa Hotel ya Oakland's Inn, Kitongoji cha Randburg, Johannesburg, Afrika Kusini wamemwelezea Mtangazaji maarufu Ephraim Kibonde jinsi walivyomfahamu wakati wa uhai wake.

Kibonde alikuwa akitumia hoteli hiyo pamoja na wenzake walipokuwa wakienda Afrika Kusini kwa shughuli za kikazi.

Wafanyakazi hao walikutana na Mwandishi wa MCL Digital, Edo Kumwembe na kuzungumza naye, huku wakionyesha hisia zao na kuwaombea familia yake kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo

Charity ambaye ni Meneja wa hoteli hiyo alizungumzia kwa namna walivyomfahamu Kibonde wakati akienda nchini humo kwa shughuli zake za kikazi.

Pia mfanyakazi mwingine wa hoteli hiyo, Bwana Hunter ambaye ni msimamizi wa hoteli alisema alimwelezea Kibonde kwa namna alivyomfahamu pia akiwaombea wanafamilia wake katika kipindi hiki kigumu.