Vunja Mbavu: Zaa-Hela: Soka la bongo bila Wema Sepetu haiwezekani
Muktasari:
Aliyekuwa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alitimuliwa na klabu hiyo wiki chache zilizopita baada ya kuifundisha kwa msimu mmoja na miezi mitatu ya msimu wa pili klabuni hapo.
Mwandishi: Haloo Papa Zaa-Hela, habari yako bana? Upo Dar, Kinshasa au Parii?
Zaa-Hela: Acha shobo wewe, kaanza habari zipi? Za kuishi kifahari Ufaransa? Au za kuja Tanzania kuwekeza kwenye ‘Akademyee ya Soka’?
Mwandishi: Yoyote. Kwanza wameshakulipa pesa yako?
Zaa-Hela: Kina nani? Kama ninhao mabeberu wa Jangwani hawana hela ya kunilipa. Labda mimi ndo niwakopeshe.Mwandishi: Umeona timu hivi sasa inashinda tu kwa pasi za kampa kampa tena. Siyo wewe na soka la kujilinda kama Masai.
Zaa-Hela: Kama mfungaji wao tegemeo nimemleta mimi, nani anapaswa kupongezwa?
Maana siyo unajisifu kuoa mke wakati anaishi kwa ubini wangu.
Mwandishi: Anayemfundisha kwa sasa. Wewe ulichokuwa unamuelekeza ni namna ya kutaua miguu na kutetemeka kabla ya kupiga faulo.
Zaa-Hela: Shubaamiti wewe... Kwanza vipi Wema Sepetu yupo? Nasikia toka niondoke anakondeana tu ndenge nini?
Mwandishi: Kwani wewe ulikuwa unampa nini? Au ulikuwa ‘sponsa’ wake?
Zaa-Hela: Yule ni fansi ya Yanga. Nilipoondoka yeye analiumua sana. Hakutaka kabisa niondoke tatizo watu wa Yanga hamjui mpira. Mnajua kelele tu.
Mwandishi: Nitake radhi mimi siyo Yanga. Halafu pili habari za Wema hazihusiani na soka.
Zaa-Hela: Tanzania bila Wema haiwezekani. Ile binti ukiitazama kwa pasii unajikuta hata jinsi ya kufundisha mpira unakosa ‘konsetreshoo’.
Mwandishi: Kwa hiyo yeye ndo alifanya uwe unajipangia timu kama nyumba vile unavaa pensi?
Zaa-Hela: Kwanza niambie nasikia kocha wa Simba naye wamemtimu?
Mwandishi: Sasa nitajuaje kama wamemtimua au katimka mwenyewe?
Zaa-Hela: Kwani.wewe si mwandishi? Na kazi ya mwandishi si kuchunguza? Au wewe unachunguza maisha yangu tu?
Mwandishi: Nachunguzaje wakati wewe mwenyewe unaropoka sana . Yaani huwezi kuweka pozi. Kabla hujapewa barua ya kuvunja mkataba ukaongea maneno mengi sana.
Zaa-Hela: Kwa hiyo wewe nini kinakuuma? Kwanza wewe ni mwanahabari gani hujui kama Kidefu Ndevu katimuliwa Simba?
Mwandishi: Hapa nashughulika na wewe acha kunitajia wasiokiwepo.
Zaa-Hela: Simba na Yanga kama minyoo. Hawaeleweki wapi mbele wapi nyuma. Mimi kudroo mechi moja kosa. Haya huyo wa Simba naye vipi anajilinda sana?
Mwandishi: Sasa wewe umekuwa mwandishi tayari unanibana na maswali?
Zaa-Hela: Nyinyi wambea tu mnasingizia mimi sijui fundisha mpira. Mkanitimua sasa huyo wa Simba naye kakosa nini? Ndo maana nasema hamjui mpira Tanzania.
Mwandishi: Wewe ulizidi bana, ulikuwa hata hujui kikosi gani cha kwanza na nani wa kumtoa na wakati gani.
Zaa-Hela: Acha ukuda ndezi wewe. Nilipokuwa nampanga kila siku Molinga mliona nampendelea. Sasa vipi hao waliobaki nao hawampangi?
Mwandishi: Unakuja lini Bongo? Simba kama kweli wamemtimua kocha si uje uchukue nafasi yake?
Zaa-Hela: Mimi siwezi fundisha timu yenye mtu tajiri zaidi yangu. Hata kule Zambia niliacha kwenda kufundisha kwa sababu kuna mtu alikuwa tajiri. Nilipoambiwa Yanga wanaishi kama yatima nikasema hapahapa.