Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita ya kimkakati Championship

CHAMPIONSHIP Pict

Muktasari:

  • Katika mechi mbili zilizochezwa jana Ijumaa KenGold iliyochapwa na Tanzania Prisons mabao 2-1 wiki iliyopita ilikuwa kwenye Uwanja wa Halmashauri ya Chunya jijini Mbeya kuikaribisha Gunners FC iliyochapwa pia na Mtibwa Sugar mabao 2-1.

RAUNDI ya 12 ya Ligi ya Championship iliendelea jana Ijumaa kwa mechi mbili kuchezwa na leo Jumamosi zikichezwa tatu na nyingine zikihitimishwa kesho Jumapili kwenye viwanja mbalimbali huku ushindani ukionekana kutawala wiki baada ya wiki.

Katika mechi mbili zilizochezwa jana Ijumaa KenGold iliyochapwa na Tanzania Prisons mabao 2-1 wiki iliyopita ilikuwa kwenye Uwanja wa Halmashauri ya Chunya jijini Mbeya kuikaribisha Gunners FC iliyochapwa pia na Mtibwa Sugar mabao 2-1.

Katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kulikuwa na vita ya maafande na Rhino Rangers iliyochapwa mabao 2-1 dhidi ya Kigamboni United ilicheza dhidi ya Transit Camp yenye kumbukumbu ya kutoka suluhu (0-0) na Stand United.

Leo, Jumamosi, zitachezwa mechi tatu na Tabora United iliyoifunga Songea United mabao 3-1 itakuwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora kucheza dhidi ya KMC FC kutoka Kinondoni Dar es Salaam iliyotoka sare ya bao 1-1 na TMA FC.

CHAMP 07

Tabora United inashika nafasi ya 14 na pointi 10 baada ya kucheza mechi 11 ikishinda tatu sare moja na kupoteza saba huku kwa upande wa KMC FC ikiwa ya tatu na pointi 20 kufuatia kushinda tano ikitoka pia sare tano na kuchapwa moja.

Tabora itaendelea kumtegemea mshambuliaji nyota wa timu hiyo Abiud Mtambuka aliyefunga mabao sita kati ya 13 ya kikosi hicho huku KMC ikimtegemea Ramadhan Hashim Kalanje aliyeifungia tisa hadi sasa na kuonyesha kiwango bora cha kuvutia.

Kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya maafande wa Tanzania Prisons iliyotoka kuichapa KenGold FC mabao 2-1 itacheza dhidi ya kikosi cha Kigamboni United chenye kumbukumbu nzuri baada ya wiki iliyopita kuifunga Rhino Rangers mabao 2-1.

CHAMP 08

Katika mechi 11 ilizocheza Prisons imeshinda saba sare mbili na kupoteza pia mbili ikishika nafasi ya pili na pointi 23 huku Kigamboni United ikiwa nafasi ya nane na pointi 15 baada ya kushinda nne ikitoka sare tatu na kupoteza nne.

Miongoni mwa nyota wa kuchungwa kwa timu zote mbili ni Oscar Paul wa Tanzania Prisons na Abdulkarim Segeja wa Kigamboni United ambao wote wamekuwa katika kiwango cha kuvutia msimu huu baada ya kila mmoja wao kufunga mabao tisa hadi sasa.

Kocha Mkuu wa Prisons Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’ amesema mwenendo wa timu hiyo kwa sasa unaridhisha na unawapa morali ya kupambana zaidi huku akiwataka wachezaji wa kikosi hicho kucheza kwa nidhamu ili kubakia na pointi zote tatu nyumbani.

CHAMP 01

“Kadri ambavyo raundi zinazidi kusogea ushindani nao unakuwa mkubwa kwa sababu ya mahitaji ya kila mmoja wetu hii ni mechi nyingine ngumu tunayoenda kucheza lakini tumejipanga vizuri kimwili na kiakili kupata ushindi,” amesema Nsajigwa.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Kigamboni United Twaha Beimbaya amesema licha ya kasi nzuri ya safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ila miongoni mwa eneo analoendelea kuliboresha zaidi ni lile la kujilinda ili kutengeneza balansi ya kiuchezaji.

“Tumekuwa na safu bora ya ushambuliaji ila changamoto yetu ni eneo la kujilinda na hilo liko wazi kwa sababu hadi sasa tumecheza mechi 11 na kuruhusu mabao 11 ikiwa na maana tunaruhusu kila mechi jambo ambalo sio nzuri,” amesema Beimbaya.

CHAMP 02

Mechi ya mwisho leo Jumamosi itachezwa kwenye Uwanja wa Aga Khan jijini Arusha na IAA SC iliyotoka sare ya bao 1-1 wiki iliyopita dhidi ya majirani zao Mbuni FC itaikaribisha Bandari Tanzania iliyochapwa na Bigman FC ya Tanga 1-0.

IAA SC iliyocheza mechi 11 imeshinda mbili sare sita na kupoteza tatu ikishika nafasi ya 13 na pointi 12 huku kwa upande wa Bandari Tanzania ikishinda tano ikitoa sare tatu na kupoteza pia tatu ikiwa nafasi ya nne na pointi zake 18.

Timu ya IAA SC ya Arusha ilifuzu kucheza Ligi ya Championship kwa msimu wa 2026-2027 kupitia mechi ya ‘Play-Off’ baada ya kuitoa African Sports ya Tanga kwa jumla ya mabao 3-2 ikishinda nyumbani 2-1 kisha ugenini ikatoka sare ya bao 1-1.

CHAMP 03

Raundi ya 12 itahitimishwa kesho Jumapili kwa mechi tatu kuchezwa na Stand United iliyotoka suluhu (0-0) dhidi ya Transit Camp itaikaribisha Songea United ikiwa na kumbukumbu mbaya baada ya kutoka kufungwa na Tabora United mabao 3-1.

Stand United ‘Chama la Wana’ katika mechi 11 ilizocheza imeshinda nne sare tatu na kupoteza nne ikiwa nafasi ya tisa na pointi 15 huku Songea United ikishinda moja sare tatu na kupoteza saba ikishika nafasi ya 15 na pointi zake sita.

Kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa TMA FC inayoburuza mkiani mwa nafasi ya 16 na pointi tatu itaikaribisha Mbuni FC kutoka jijini Arusha inayoingia katika mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya IAA SC.

CHAMP 04

TMA FC iliyohamishia makazi yake mjini Iringa ikitokea Arusha imekuwa na mwenendo usioridhisha hadi sasa baada ya timu hiyo kushinda mechi moja tu kati ya 11 iliyocheza ikiwa na kibarua kigumu cha kupigania nafasi ya kubaki Championship.

Kuonyesha timu hiyo ina kazi kubwa ya kupigania kutoshuka daraja safu ya ushambuliaji imefunga mabao manne hadi sasa huku eneo la kujilinda likiruhusu 17 ikiwa ni wastani wa kuruhusu bao katika kila mechi inayocheza tangu msimu umeanza.

Bigman FC iliyoishangaza Bandari Tanzania kwa kuifunga bao 1-0 itakuwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kucheza dhidi ya vinara wa Ligi hiyo Mtibwa Sugar iliyotoka kuichapa Gunners FC ya jijini Dodoma mabao 2-1 wiki iliyopita.

Mtibwa Sugar inaongoza ikiwa na pointi 24 baada ya kushinda mechi saba sare tatu na kupoteza moja kati ya 11 za msimu huu huku kwa upande wa Bigman ikishinda tano sare moja na kupoteza tano ikishika nafasi ya saba na pointi zake 16.