Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo wawili wakwama uchaguzi Yanga

Muktasari:

  • Gulamali na Gumbo walikuwa ni miongoni mwa viongozi watano waliokuwa wakitetea nafasi zao za Kamati ya Utendaji ya Yanga kwa kipindi cha miaka minne mingine ijayo.

VIGOGO wawili waliokuwa katika Kamati ya Utendaji ya Yanga, Seif Gulamali na Rodgers Gumbo, wameshindwa kutetea nafasi zao katika Uchaguzi Mkuu wa Yanga uliofanyika Jumapili ya Agosti 2, 2026, kwenye Ukumbi wa The Super Dome uliopo Masaki jijini Dar es Salaam.

Gulamali na Gumbo walikuwa ni miongoni mwa viongozi watano waliokuwa wakitetea nafasi zao za Kamati ya Utendaji ya Yanga kwa kipindi cha miaka minne mingine ijayo.

Akitangaza matakeo ya wajumbe walioteuliwa, Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Yanga, Malangwe Mchungahela, amesema walioshinda nafasi hizo tano ni Yanga Makaga aliyepata kura 526, Alex Ngai (kura 519), Julius Koyi (kura 500), Munir Said (kura 439) na Farid Afif (kura 438).

Kati ya hao watano walioshinda, wawili wapya waliopenya ni Julius Koyi na Farid Afif na kuwatoa Gumbo na Gulamali waliokuwepo katika awamu iliyopita.

Kwa upande wa Gulamali, alipata kura 422, huku Gumbo akipata kura 327, kati ya 817, zilizopigwa na wanachama wa Yanga.

Matokeo mengine, Issa Mangungu alipata kura 358, Injinia Mustapha Himba (kura 125), Prisca Kishamba (kura 103), Mshindo Hamza Msola (kura 172), Saady Khimji (kura 73), Freddy Mahembe (kura 21), Mzee Yusuph (kura 32) na Mohammed Mwenda (kura 25).

Uongozi mpya wa Yanga uliochaguliwa kuunda Kamati ya Utendaji kwa kipindi cha miaka minne ijayo kuanzia leo unaongozwa na Rais, Injinia Hersi Said na Makamu wake, Arafat Haji waliotetea nafasi zao huku wakiingia kwenye uchaguzi huo bila mpinzani. Wajumbe ni Yanga Makaga, Alex Ngai, Julius Koyi, Munir Said na Farid Afif.