Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hersi avunja makundi uchaguzi Yanga

Muktasari:

  • Hersi ametangaza hayo wakati akihutubia wanachama wa mkutano huo mkuu uliofanyika Agosti 2, 2026 na kumalizika usiku huu.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, amewataka wanachama wa klabu hiyo kuvunja makundi na kambi za uchaguzi uliomalizika.

Hersi ametangaza hayo wakati akihutubia wanachama wa mkutano huo mkuu uliofanyika Agosti 2, 2026 na kumalizika usiku huu.

Rais huyo ambaye ametetea kiti chake, amesema wagombea ambao wameshindwa, hawatakiwi kuyachukua matokeo hayo kwa chuki kwani wao bado ni wanachama wa Yanga.

"Niwapongeze wagombea ambao wamefanikiwa kurudi kwenye Kamati ya Utendaji, nawaona watatu lakini kuna wawili wapya wameingia, karibuni sana," amesema Hersi.

"Wagombea ambao wamekosa nafasi nao ni washindi hata kama kura hazijatosha, hawatakiwi kugeuka maadui wa klabu yetu, wao bado ni wanachama wanatakiwa kuwa sehemu ya klabu yao."

Aidha, Hersi amewataka wanachama wa klabu hiyo nao kuvunja makundi yao na kurudisha nguvu ya umoja kwenye kuipigania Yanga kwenye miaka minne ijayo.

"Wanachama wenzangu nanyi nawataka kuvunja kambi zote huko kwenu, kama mgombea wako ameshindwa au ameshinda nyie wote ni wanachama wa Yanga na sio mtu mmoja, turudi kuunganisha nguvu kuipigania klabu yetu," amesema.

Safu mpya ya uongozi wa Yanga itaongozwa na Hersi, Makamu wake akiendelea kuwa Arafat Haji, wakati wajumbe waliopenya ni Yanga Makaga, Alexander Ngai, Munir Seleman, Julius Koyi na Fahd Afif.