Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIBEN TEN: Mastaa wa soka wenye wake wakubwa kiumri

Muktasari:

  • Jambo hilo linadaiwa kuvamia pia kwenye soka la Ulaya, ambapo mastaa wa soka kibao wa maana wamejikuta wakiingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanawake wenye umri mkubwa kuliko wao.

WANASEMA hivi mapenzi hayana umri. Kwa miaka ya karibuni, umeibuka utamaduni wa wanawake mwenye umri mkubwa kuolewa au kuanzisha uhusiano wa kipenzi na wanaume wenye umri mdogo.

Jambo hilo linadaiwa kuvamia pia kwenye soka la Ulaya, ambapo mastaa wa soka kibao wa maana wamejikuta wakiingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanawake wenye umri mkubwa kuliko wao.

Hawa hapa mastaaa watano walioa wanawake wenye umri mkubwa kuliko wao.

5.Icardi na Wanda Nara- miaka 6

Mrembo, Wanda Nara mwenye umri wa miaka 29, alimtosa swahiba wa mshambuliaji Mauro Icardi, ambaye walikuwa wakicheza timu moja, Maxi Lopez na kuanzisha uhusiano na staa huyo wa Inter Milan mwaka 2013. Icardi umri wake ni miaka 23, hivyo kwa maana hiyo, amezidiwa miaka sita kwenye uhusiano wao.

Icardi hakutazama suala la umri na kuamua kuingia kwenye uhusiano naye na sasa analea tu watoto wa swahiba wake wa zamani Maxi Lopez.

4.Ramos na Pilar Rubio- miaka 8

Beki, Sergio Ramos, 32, ameingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mwandishi wa Habari na Mtangazaji, Pilar Rubio, 40, Septemba 2012 ambao wawili hao walithibitisha hilo walipokwenda kwenye sherehe za tuzo za Fifa Ballon d’Or. Wawili hao hawakujali tofauti ya umri wao, hasa kwa mwanamke kuwa mkubwa kwa miaka minane dhidi ya mwanamume, wameingia kwenye mahaba mazito na kufanikiwa kupata watoto watatu wa kiume, Sergio, Marco na Alejandro.

3. Pique na Shakira- miaka 10

Wote wanafanya vizuri na kufanikiwa kwenye biashara zao walizochagua kufanya.

Beki Gerard Pique mwenye umri wa miaka 31 amekuwa na mafanikio makubwa kwenye kikosi cha Barcelona na Timu ya Taifa ya Hispania, wakati mrembo Shakira, mwenye uhusiano naye, ana umri wa miaka 41.

Mrembo huyo wa Colombia ni mwimbaji. Wawili hao wamefanikiwa kupata watoto wawili, Milan na Sasha.

2. Fabregas na Daniella Semaan- miaka 11

Siku si nyingi tu hapo, kiungo wa Chelsea, Mhispaniola Cesc Fabregas alifunga pingu za maisha na mama watoto wake, mrembo Daniella Semaan. Sherehe ya harusi yao ilifanyika huko Ibiza. Umri wa Fabregas kwa sasa ni miaka 31, lakini mwanamke wake aliyeona naye amemzidi kwa miaka 11.

Wawili hao wamefanikiwa kupata watoto watatu, wa kike wawili, Lia na Capri na wa kiume mmoja, Leonardo. Lakini, ndiyo hivyo, wawili hao mume ana miaka 31, mke miaka 42.

1.Zlatan na Helena Seger- miaka 12

Supastaa Zlatan Ibrahimovic kwa sasa umri wake ni miaka 36, lakini mke wake aliyemwoa, mrembo Helena Seger umri wake ni miaka 48. Kuna tofauti na miaka 12 baina yao. Helena ni mfanyabiashara.

Wawili hao walikutana mwaka 2002, kipindi hicho Ibra alikuwa na umri wa miaka 20 na Helena miaka 32. Miaka minne baada ya kukutana, wakapata mtoto wao wa kwanza wa kiume, Maximilian na mwaka 2008, wakapata mtoto wa pili wa kiume, Vincent. Zlatan na Helena pia wana mbwa wao anaitwa Trustor.