Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uwanja wa Afcon wafikia asilimia 65

AFCON Pict

Muktasari:

  • Kauli hiyo aliitoa, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya AFCON 2027 katika Uwanja wa Fumba pamoja na viwanja vya Matemwe na Matumbaku.

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Riziki Pembe Juma, amesema ujenzi wa mradi wa Uwanja wa michezo wa Zanzibar (Fumba Studium) unaendelea vizuri na hakuna sehemu ya mradi iliyosimama hadi sasa, huku ikibainishwa umefikia asilimia 65.

Kauli hiyo aliitoa, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya AFCON 2027 katika Uwanja wa Fumba pamoja na viwanja vya Matemwe na Matumbaku.

Amesema, Serikali imejipanga kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati uliopangwa hivyo amewataka wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi kwa kuzingatia viwango bora vya kimataifa.

AFCO 02

Waziri Riziki, alimpongeza Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi, kwa hatua kubwa anazoendelea kuchukua katika kuimarisha miundombinu ya maendeleo.

Amesema, Rais Mwinyi anaendelea kuimarisha sekta ya michezo kupitia ujenzi wa miundombinu ya kisasa hivyo awasihi wananchi kuitunza ili iweze kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.

Aidha, aliwahimiza wananchi kujiandaa kunufaika na fursa za kiuchumi zitakazotokana na mashindano hayo, zikiwemo ujasiriamali, utalii na biashara mbalimbali za huduma kwa wageni watakaotembelea nchini.

AFCO 01

Kwa upande wake, Mshauri Elekezi wa mradi kutoka kampuni ya Orkum Group. Simbo Nkya, amesema ujenzi wa uwanja wa Fumba umefikia asilimia 65 na unatarajiwa kukamilika kwa wakati uliopangwa, huku ukikidhi viwango vinavyotakiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).