Ukame wa mabao wampa shida straika wa IAA SC
Muktasari:
- Alijiunga na IAA SC msimu huu wa 2026/27 akitokea Mbeya Kwanza, ambayo kwa sasa inatumia jina la Tabora United. Katika msimu uliopita wa 2025/26, akiwa na timu hiyo, alifunga mabao 11.
MSHAMBULIAJI wa IAA SC, Boniface Mwanjonde, amesema kutofanya vizuri katika mwanzo wa msimu na kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza ni miongoni mwa sababu zilizochangia kupungua kwa kasi yake ya kufunga mabao.
Akizungumza na Mwanaspoti, Mwanjonde amesema alikutana na changamoto ya kuzoea kikosi kipya baada ya kujiunga na timu hiyo, lakini kwa sasa ameanza kupata nafasi zaidi ya kucheza, jambo linalompa motisha ya kuendelea kupambana.
“Nimejiunga na timu mpya na wachezaji niliokutana nao hapa ni wapya pia. Ushindani ni mkubwa, lakini nahitaji kujituma zaidi ili benchi la ufundi liendelee kuniamini na kunipa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza. Hivyo, sijakata tamaa,” amesema.
Mwanjonde, ambaye hadi sasa amefunga mabao mawili, amesema licha ya mwanzo kuwa mgumu, ameanza kuzoea mazingira ya timu hiyo na kuona maendeleo katika kiwango chake cha uchezaji.
Amesema hali hiyo inampa hamasa ya kuongeza juhudi ili kurejesha makali yake ya kufunga mabao na kuisaidia timu kupata matokeo mazuri.
Mshambuliaji huyo aliwahi kuzichezea KenGold, Ndanda na Mbeya City chini ya miaka 20, kabla ya kwenda Chitipa United ya Malawi.
Alijiunga na IAA SC msimu huu wa 2026/27 akitokea Mbeya Kwanza, ambayo kwa sasa inatumia jina la Tabora United. Katika msimu uliopita wa 2025/26, akiwa na timu hiyo, alifunga mabao 11.