Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kichudi aula Uhamiaji

KICHUDI Pict
KICHUDI Pict

Muktasari:

  • Mabadiliko hayo ya benchi la ufundi yanakuja baada ya Oktoba 30, 2026, Uhamiaji kulivunja benchi lote lililokuwa likiongozwa na Kocha Mkuu, Sheha Khamis kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya.

KOCHA wa zamani wa Fufuni, Salum Haji ‘Kichudi’ ametua Uhamiaji akiwa kocha msaidizi, akichukua nafasi ya Hassan Makame Ameir aliyeondoka katika benchi la ufundi la timu hiyo kutokana na mabadiliko yaliyofanywa na uongozi.

Kichudi ambaye tayari ameanza kazi katika kikosi hicho, ametua wakati Uhamiaji ikionyesha dalili za kurejea kwenye makali yake baada ya kupata ushindi wa mechi mbili mfululizo katika Ligi Kuu Zanzibar (ZPL).

Mabadiliko hayo ya benchi la ufundi yanakuja baada ya Oktoba 30, 2026, Uhamiaji kulivunja benchi lote lililokuwa likiongozwa na Kocha Mkuu, Sheha Khamis kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya.

KICHU 01

Ingawa klabu hiyo haijatoa taarifa rasmi kuhusu uteuzi wa Kichudi, lakini Mwanaspoti ilimshuhudia kocha huyo akiwa kazini katika mchezo dhidi ya Mlandege, ambao Uhamiaji iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kichudi amesema ushindi huo umetokana na maandalizi mazuri pamoja na mpango wa timu kuanza mchezo kwa kasi ili kupata mabao mapema na kuwadhibiti wapinzani.

Amesema walilenga kutumia dakika 30 za kipindi cha kwanza kutengeneza mabao huku wakihakikisha wanailinda vyema ngome yao ili kutoruhusu wapinzani kupata nafasi ya kurejea mchezoni.

KICHU 02

"Wachezaji wameamua kurejea katika timu na kucheza kwa nidhamu pamoja na tahadhari. Hiyo ndiyo siri kubwa inayotusaidia kupata matokeo mazuri katika michezo ya hivi karibuni," amesema Kichudi.

Hata hivyo, amesema licha ya ushindi huo, bado kuna upungufu kikosini unaopaswa kufanyiwa kazi ili kuimarisha zaidi kikosi hicho katika michezo ijayo.

Ametaja eneo la ushambuliaji ni miongoni mwa sehemu zinazohitaji maboresho na wachezaji wamekuwa wakikosa utulivu na umakini wanapopata nafasi za wazi za kufunga.

Pia, amesema safu ya ulinzi inapaswa kuongeza umakini katika kutekeleza majukumu yake ili kuifanya timu iwe imara katika maeneo yote ya uwanja.

KICHU 03

Aidha, aliwataka mashabiki wa Uhamiaji kurejea kuisapoti timu yao kwa kujitokeza kwa wingi viwanjani na hali ya furaha imeanza kurejea ndani ya kikosi hicho na hakuna sababu ya kuikatia tamaa.

Uhamiaji imekusanya pointi sita katika michezo miwili iliyopita, baada ya kuichapa Muembe Makumbi mabao 2-1 kabla ya kuizamisha Mlandege 3-0.

Matokeo hayo yameifanya timu hiyo kufikisha pointi 23 na kupanda hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, ikiwa na pointi sawa na KMKM inayoshika nafasi ya nne.