Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ujanja wa Pantev akianza kuinoa Simba 

PANTEV Pict


KOCHA mpya wa Simba, Dimitar Pantev aliyetambulishwa kama meneja siku chache zilizopita, ametua Msimbazi akiwa na mtazamo tofauti wa kimbinu na Fadlu Davids unaolenga kuongeza ubora.


Kutokana na tathmini yake ya awali ya wachezaji, Pantev ameeleza kuridhishwa kwa zaidi ya asilimia 80 na kikosi akibaini wachezaji wengi wana sifa zinazolingana na mtindo wake wa uchezaji.


Hali hii inaonyesha falsafa za Pantev zinazingatia ubora wa mchezaji mmoja mmoja ili kuunda timu yenye uwiano mzuri katika kutengeneza mashambulizi yenye kasi na umiliki wa mechi, jambo ambalo ameonakana kulihitaji ili kurejesha heshima ya Mnyama.

Pantev aliyetokea Gaborone United ya Botswana ana kibarua cha kuendeleza alichofanya Fadlu aliyetimkia Raja Casablanca kwa kufanya vizuri michuano ya kimataifa na ndani ambako wameambulia patupu kwa misimu minne.

PANTE 01

HUYU HAPA

Katika mahojiano ya awali na Mwanaspoti, kocha huyo anasema: “Nilichokiona kwa wachezaji mmoja mmoja kimenipa matumaini. Hii ni timu yenye vipaji vikubwa kila mmoja ana kitu cha tofauti.”

Pantev anaeleza falsafa yake kubwa inajikita kuhakikisha kila kipaji kinatumika vizuri ndani ya mfumo wa timu na kunakuwa na uwiano mzuri katika kushambulia na kujilinda.Hilo linaweza kuifanya Simba kuwa moto wa kuotea mbali.

“Msingi wa soka langu ni kucheza kwa kushambulia zaidi huku tukiwa na umiliki wa mchezo,” anasema.

PANTE 02

TOFAUTI KIMFUMO

Tofauti kubwa kati ya Pantev na Fadlu ni mfumo.  Fadlu alikuwa akitumia 4-2-3-1 ukilenga uwiano kati ya kulinda na kushambulia huku viungo wawili wa kati wakichukua jukumu kubwa la kulinda na katika hilo kwa msimu uliopita, Fabrice Ngoma na Yusuph Kagoma walifanya vizuri zaidi.

Pantev, kwa upande wake ni muumini 4-3-3 unaojikita kushambulia moja kwa moja kupitia winga na mshambuliaji wa kati mmoja, huku viungo watatu wa kati wakiwa na jukumu la kusukuma timu mbele na kuhakikisha uwiano wa kati haupotei.

Mfumo huounalenga kuongeza kasi ya mashambulizi, kutoa nafasi kwa mawinga na washambuliaji kushambulia, kitu ambacho kina-we-za kuwafanya wapinzani kuwa na wakati mgumu ikiwa watashindwa kukabiliana na presha ya mashambuliizi hayo.

Mbali na kupendelea kutumia mfumo wa 4-3-3, Pantev ni mtaalamu wa mbinu za kisasa ambaye hubadilika kulingana na mazingira ya mchezo. Kuna nyakati ambapo huamua kutumia mfumo wa mabeki watatu (3-4-3 au 3-5-2) ili kuongeza usalama wa ulinzi na nguvu eneo la kiungo. Mabadiliko hayo hutegemea aina ya wapinzani, uimara wa wachezaji na matokeo anayoyahitaji katika mchezo husika.


ISHU ILIPO

Kocha huyo anathamini uwezo wa wachezaji kumiliki mpira, kusuka mashambulizi na kutengeneza nafasi kwa washambuliaji wa mwisho kama Jonathan Sowah, Seleman Mwalimu na Steven Mukwala.

Wachezaji kama Ellie Mpanzu, Charles Jean Ahoua, Kibu Denis, Morice Abraham, Joshua Mutale, Ladack Chasambi na Mohammed Bajaber (ambaye yupo njiani kurejea) wanachukuliwa kuwa silaha muhimu katika falsafa hii.  Uwezo wao wa kuunganishwa na mfumo wa 4-3-3 utalenga kuhakikisha timu inashambulia haraka, kuwa na nafasi nyingi za kufunga na kudhibiti kushambuliwa kuanzia juu.

PANTE 03

UWIANO KIMFUMO

Falsafa za Pantev hazizingatii kushambulia tu. Kocha huyo ana mtazamo kwamba timu lazima iwe na namna nzuri ya kujilinda.

Wachezaji wanapaswa kushirikiana katika kuzuia mashambulizi ya wapinzani wao huku wakiwa tayari kushambulia. Historia yake inaonyesha mafanikio makubwa katika kuunda timu zenye wastani wa kufunga mabao karibu mawili kwa mechi, huku zikiruhusu bao chache. Msimu uliopita akiwa na Gaborone aliifanya timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi huku ikifunga jumla ya mabao 56 katika mechi 30.


KAANZIA HAPA 

Safari ya kwanza ya kikosi kuelekea Eswatini kwa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nsingizini Hotspurs itakuwa jaribio la kwanza la utekelezaji wa falsafa ya Pantev.

Mechi za kirafiki kabla ya safari ikiwemo dhidi ya Al Hilal ya Sudan, zilijikita kuhakikisha wachezaji wanapata mazoezi ya utekelezaji wa mashambulizi ya haraka, umiliki wa mchezo na uwiano wa timu.

Pantev anaamini hatua kidogo kidogo za kuingiza falsafa zake ni muhimu, kuanzia kuunda mfumo unaojumuisha uwezo wa kila mchezaji wakati ambao Simba inahitaji kutinga makundi ya michuano hiyo ya kimataifa.