Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uganda kujiuliza mbele ya Guinea

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo ya Kundi C itakayopigwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Uganda itakuwa inasaka pointi za kwanza kama wenyeji wa michuano hiyo sambamba na Kenya na Tanzania ambazo zenyewe zilianza kibabe mechi zao katika Makundi A na B, kwani ilipoteza 3-0 kwa Algeria.

TIMU ya taifa ya Uganda The Cranes, inashuka tena uwanjani leo kutupa karata ya pili ya Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji Wanaocheza Ligi za ndani (CHAN), itakaposaka ushindi wa kwanza mbele ya Guinea, pambano litakaloanza saa 2:00 usiku.

Katika mechi hiyo ya Kundi C itakayopigwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Uganda itakuwa inasaka pointi za kwanza kama wenyeji wa michuano hiyo sambamba na Kenya na Tanzania ambazo zenyewe zilianza kibabe mechi zao katika Makundi A na B, kwani ilipoteza 3-0 kwa Algeria.

Wapinzani wao, walianza kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Niger, kitu kinachofanya pambano la leo kuwa ni vita ya aina yake kwa wenyeji mbele ya Guinea.

Kichapo hicho cha Uganda cha mabao 3-0 kutoka kwa Algeria, kimeifanya The Cranes kupoteza pambano la 11 la mechi ya ufunguzi kati ya 19 za CHAN, ambapo kimeshinda mbili tu na kutoka sare sita, huku kikiwa hakijashinda mechi mbili za makundi.

Uganda haijawahi kushinda mechi mbili za hatua ya makundi kati ya mara nne ilizoshiriki michuano ya CHAN kuanzia mwaka 2011, 2016, 2018 na 2020 jambo linalosubiriwa kuona kile kitakachojiri pia leo wakati ikisaka ushindi wake wa kwanza.

Kwa upande wa Guinea, haijapoteza mechi nane za CHAN zilizopita ambapo kati ya hizo imeshinda nne na kutoa sare pia nne, ingawa mtihani mgumu inaoenda kukabiliana nao leo ni rekodi mbovu iliyonayo ya kushindwa kushinda mechi mbili mfululizo.

Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana ilikuwa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia, ambapo mechi hiyo ya kwanza ya kundi F, Guinea ilishinda mabao 2-1, Novemba 17, 2023, japo Uganda ililipa kisasi nyumbani baada ya kushinda 1-0, Machi 25, 2025.

Katika kundi hilo la F, Algeria iliongoza na kufuzu kwa pointi 15, ikifuatiwa na Msumbiji iliyomaliza ya pili na pointi 12, huku Botswana na Uganda zikimaliza za tatu na nne na pointi tisa kila mmoja, wakati Guinea ilikuwa ya tano na pointi saba.

Kwenye kundi hilo, timu ya Taifa ya Somalia iliburuza mkiani na pointi moja tu, baada ya kupoteza mechi tano na kutoka sare moja kati ya sita ilizocheza, huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao matatu na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 11.

Mechi nyingine ya kundi C, itakayopigwa mapema saa 11:00 jioni uwanjani hapo pia, kati ya Algeria itakayoonyeshana kazi na Afrika Kusini ambayo inaanza rasmi kufungua pazia la michuano hiyo ya CHAN 2024.

Mechi ya mwisho kwa timu hizo kukutana ilikuwa ni ya kirafiki iliyopigwa Machi 27, 2024, ambapo zilitoka sare ya mabao 3-3, ingawa za kimashindano zilikutana katika Mataifa ya Afrika (AFCON) na Algeria kushinda mabao 3-1, Januari 19, 2015.