Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TTB kusapoti soka la wanawake Kigoma ikilenga kuhamasisha utalii

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imedhamiria kutumia mpira wa miguu hasa kwa wanawake kutangaza na kuhamasisha utalii wa ndani na mataifa yaliyo katika jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hilo limekuja kufuatia kuongezeka kwa mwingiliano wa watu wa nchi hizo za Afrika Mashariki unaochagizwa na michezo hasa mpira wa miguu.

Mkurugenzi wa TTB Felix John ameyasema hayo wakati akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya mpira wa miguu ya Mwanga Queens iliyopo mkoani Kigoma.

Amesema Kigoma ni mkoa wa kimkakati umepakana na nchi za Rwanda, Burundi na DRC hivyo ukiwekewa mikakati mizuri unaweza kuhamasisha watu wengi wa nchi hizo.

Felix amesema kutokana na hilo TTB imeona ipo haja ya kutoa jezi kwa timu hiyo zikiwa na chapa za kutangaza utalii wa Tanzania ili zitumike kwenye ambayo timu hiyo ya wanawake inashiriki.

“Michezo ni kati ya mazao ya utalii ambayo tuna jukumu la kuyaendeleza, tumeangalia Kigoma ni mkoa wa kimkakati hivyo tuna kila sababu ya kuutumia vyema ili kukuza utalii wa kikanda. Kwa utalii tunaona hapa ni sehemu sahihi,”.

Akizungumzia msaada  huo kocha wa timu ya Mwanga Queen Kashinde Manga amesema vifaa hivyo vitakuwa chachu ya wachezaji kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa mpira wa miguu.

“Tutaenda kuwa mabalozi wazuri, huwa tunasafiri kwenda kucheza mechi za kirafiki Burundi hivyo kupata jezi ambazo zinatangaza vivituo vyetu itakuwa fursa pia kwetu kushiriki kwenye uhamasishaji huu na kuwavuta zaidi watalii kutoka nchi jirani kuja hapa nchini,” amesema Manga.