Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TRA United kuchomoa mtaalamu Yanga

TRA Pict

Muktasari:

  • Mbali na nafasi hiyo ya kikosi cha kwanza, Bartalomew amewahi pia kuhudumu akiwa kocha mkuu wa timu ya Yanga ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (Head Coach U-17) na Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana, ambapo kwa sasa ana uzoefu mkubwa.

UONGOZI wa TRA United umeanza mazungumzo ya kupata huduma ya Mtaalamu wa Uchambuzi wa Utendaji wa Wachezaji (Performance & Tactical Analyst) wa Yanga, Bartalomew Prosper, ikiwa ni mchakato wa kuongeza nguvu katika benchi la ufundi kikosini.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo, zimeliambia Mwanaspoti, Bartalomew ni miongoni mwa mapendekezo ya benchi la ufundi la kikosi hicho chini ya Kocha Mkuu, Hemed Suleiman ‘Morocco’ anayepambana kuhakikisha anarejesha heshima kikosini humo.

Morocco aliyefundisha klabu za Simba, Namungo FC na Geita Gold kwa Bara na timu ya taifa ya Taifa Stars, alijiunga na TRA United, Septemba 10, 2026, akichukua nafasi ya Mrundi, Etienne Ndayiragije, aliyeondoka kikosini Septemba 7, 2026.

Bartalomew amefanya kazi ya Uchambuzi wa Mbinu na Utendaji (Tactical & Performance Analyst), kisha Mkuu wa Kitengo cha Utendaji wa Timu za Vijana (Head of Performance and Youth Category) na Kocha Mkuu wa vijana chini ya miaka 17 wa Yanga.

Mtaalamu huyo amepata sifa kutokana na kazi yake katika timu za vijana na benchi la ufundi la Yanga, jambo linalopelekea uongozi wa TRA United kufanya mazungumzo kwa lengo la kuongeza nguvu ili kuimarisha ufanisi wa kikosi hicho msimu huu.

Mbali na nafasi hiyo ya kikosi cha kwanza, Bartalomew amewahi pia kuhudumu akiwa kocha mkuu wa timu ya Yanga ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (Head Coach U-17) na Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana, ambapo kwa sasa ana uzoefu mkubwa.

Pia, mtaalamu huyo amefanya kazi na makocha mbalimbali wa kikosi hicho cha wakubwa wakiwemo, Miguel Gamondi, Sead Ramovic, Miloud Hamdi na Romain Folz, jambo linalomuweka katika nafasi nzuri zaidi ya utendaji wake kutokana na uzoefu aliopata.