Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele aweka mikakati mipya TRA United

Muktasari:

  • Nyota huyo alijiunga na TRA United, Julai 25, 2026 kwa mkataba wa miaka miwili, baada ya kuachana na Mtibwa Sugar ambayo imeshuka daraja kufuatia kikosi hicho kumaliza nafasi ya 15 na pointi 27, katika Ligi Kuu kwa msimu wa 2025-2026.

MSHAMBULIAJI wa TRA United, Kassim Shaibu ‘Mayele’ amesema licha ya ugeni wake katika kikosi hicho ila hadi sasa kuna maendeleo mazuri, ingawa amekiri anapaswa kupambana ili kuendana na ushindani mkubwa kutoka kwa washambuliaji wenzake.

Nyota huyo alijiunga na TRA United, Julai 25, 2026 kwa mkataba wa miaka miwili, baada ya kuachana na Mtibwa Sugar ambayo imeshuka daraja kufuatia kikosi hicho kumaliza nafasi ya 15 na pointi 27, katika Ligi Kuu kwa msimu wa 2025-2026.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mayele alisema licha ya kupewa dakika chache za kucheza ila anaendelea kuzoea mazingira na jinsi ya kutengeneza muunganiko mzuri na washambuliaji wenzake, jambo linalompa nguvu ya kupambana ili acheze pia zaidi.

“Kwa dakika chache ninazoendelea kuzipata nataka nihakikishe nazitumia vizuri, kwa sasa tuna benchi pia jipya la ufundi, hivyo ni wakati wa kila mchezaji kuonyesha kipaji chake ili ashawishi kupewa nafasi zaidi uwanjani,” alisema Mayele.

Aidha, mshambuliaji huyo alisema licha ya kutofunga bao lolote hadi sasa la Ligi Kuu Bara, ila bado hajakata tamaa kwa sababu ni mapema, huku lengo lake kubwa ni kuhakikisha anafanya vizuri zaidi na kuivunja rekodi ya msimu wa 2025-2026.

Kwa msimu wa 2025-2026, katika Ligi Kuu Bara akiwa na Mtibwa Sugar, Mayele alihusika na mabao matatu kati ya 25 yaliyofungwa na kikosi hicho, baada ya mshambuliaji huyo kufunga mawili na kuchangia bao lingine moja kwa maana ya kutoa asisti.