Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TP MAZEMBE VS SIMBA , EL HODOUD VS YANGA

Patrick Phiri

MWANDISHI WETU SHIRIKISHO la soka Afrika (CAF) imetoa ratiba ya michuano ya kimataifa kwa kuzipangia Simba na Yanga mechi nyepesi za kuanzia lakini baada ya hapo ni lawama. Simba ikivuka itakuwa mikononi mwa TP Mazembe na Yanga itaangukia kwa Haras El Hodoud. Mazembe ya DR Congo (DRC) ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo ambayo wiki iliyopita walicheza Fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia na kufungwa mabao 3-0 na Inter Milan ya Italia wakati Haras El Hodoud ya Misri iliiondoa Simba kwa jumla ya mabao 6-3 mwaka huu kwenye Kombe la Shirikisho. Yanga na Simba kwani inakwenda DRC ambako Yanga ilitolewa na Lupopo ya huko kwenye raundi ya kwanza ya michuano hiyo mwanzoni mwa mwaka huu. Simba itaanzia harakati za michuano ya Ligi hiyo ya Mabingwa ugenini kwa kuivaa Elan Club de Mitsoudje ya Comoro kati ya Januari 28 na 30 huku Yanga ikiivaa Dedebit ya Ethiopia tarehe hizohizo kwenye Kombe la Shirikisho yenyewe ikianzia jijini Dar es Salaam. Mshindi kati ya Simba na Elan ataivaa Mazembe ambayo itaanza raundi ya pili ya michuano hiyo huku mshindi wa Yanga na Dedebit akiivaa Hodoud, ambayo ilifika kwenye hatua ya makundi katika mashindano hayo mwaka huu. Timu za Elan na Dedebit hazina historia ya kutisha na mashindano ya klabu barani Afrika na ni wazi Simba na Yanga zina nafasi kubwa ya kutinga kwenye raundi ya kwanza. Mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi aliiambia Mwanaspoti jana kuwa hawatishiki na timu yoyote ikiwemo TP Mazembe ambao ni mabingwa watetezi; "Hatuhofii timu yoyote tuko tayari kuanza mashindano, na hata hiyo Mazembe, rekodi yao haitutishi, tunataka kushangaza Dunia. Ingawa tunajua kwamba watu wengi watabeza kutokana na rekodi za Mazembe." Itakuwa mara ya pili kwa Simba kukutana na timu ya DRC tangu iliposhiriki mashindano hayo mara ya kwanza mwaka 1974. Mara ya kwanza kukutana na Wakongomani ilikuwa mwaka 1977 ilipotolewa na Vita baada ya kufungwa 1-0, mechi zote mbili zilizochezwa Dar es Salaam na Kinshasa. Katika mwaka huo, Simba ilianza na timu ubwete ya Vautour ya Gabon na kuitoa katika raundi ya kwanza. Kocha wa Yanga, Kosta Papic alisema jana kuwa; "Nimeisikia tu ratiba lakini sijakaa nikaiangalia nipe muda niiangalie, ila siifahamu Dedebit kiundani ili mradi tupo kwenye mashindano tutapambana." Yanga, ambayo imeanza kushiriki mashindano ya klabu ya Afrika tangu mwaka 1969, haijawahi kuitoa timu ya Misri ikiwa na kumbukumbu za kutolewa na miamba kama Al-Ahly, Zamalek na Ismailia. Zanzibar Ocean View ambao ni mabingwa wa Zanzibar wamepangwa na AS Vita ya DRC huku KMKM inayoshiriki Kombe la Shirikisho ikipangwa na DCMP ambayo pia ni kutoka DRC.