Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tishio jipya Simba

SIMBA Pict


TAARIFA inayopasua vichwa vya makocha na mabosi wa Simba kwasasa ni juu ya kuumia goti kwa kipa wao namba moja Djibrilla Kassali katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, lakini kama hujafahamu makipa wanne wa Wekundu hao wamekumbana na jeraha la eneo moja pekee.


Kassali aliumia dakika ya 82, wakati Simba ikishinda 2-0 ugenini dhidi ya Kagera Sugar, na nafasi yake kuchukuliwa na Hussein Abel.


Akizungumzia hilo meneja wa habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kipa huyo hajaumia kiasi cha kuhitaji upasuaji, lakini atakuwa nje kwa siku kadhaa na uhakika ni kwamba anaweza kukosa mchezo ujao wa ligi wa ugenini dhidi ya Pamba Jiji.

SIMB 02

“Kassali maendeleo yake sio mabaya, tunachoshukuru ni kwamba amepata jeraha ambalo halitahitaji kufanyiwa upasuaji zaidi ya kupatiwa matibabu ya kawaida eneo la goti, ukiliangalia lile tukio unaweza kuona kama lilikuwa rahisi lakini alipata tatizo aliposhuka chini,” amesema Ahmed.

“Mchana huu tunaondoka hapa Bukoba tukielekeka Mwanza, kwenye mchezo dhidi ya Pamba, tunaweza kumkosa (Kassali) kwenye mechi hiyo, lakini mchezo wetu wa tatu itakuwa asilimia 50 kwa 50 itategemea na maendeleo yake.

Wakati Ahmed Ally akisema hayo presha kubwa ni kwamba Kassali anakuwa kipa wa tatu kuumia goti katika majeraha ya makipa wa timu hiyo, hali inayozidi kuitafuna klabu hiyo.

Rekodi za majeruhi wa goti alianza kwa Ayoub Lakred raia wa Morocco, akafuata Ayoub Suleiman ambaye ndani ya muda mfupi akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa alipaya majeraha.

Shida hiyo ikahamia kwa Mousa Camara akikaa nje kwa muda mrefu kutokana na changamoto hiyo hiyo ambapo makipa hao wote wameshaondoka klabuni hapo kwa kukosa sehemu kubwa ya kuitumikia timu hiyo sasa ni zamu ya Kassali.

SIMB 03

Fisiotherapist Bingwa Gilbarte Kigadye akizungumzia jeraha hilo la goti kwa makipa, amesema linatokana na aina ya mazoezi mazito ya makipa ambapo yanahitaji utayari wa kiwango kikubwa wa mwili kuweza kumudu mzigo wa mazoezi hayo.

“Unajua makipa wana mazoezi magumu sana ambayo yanahitaji utimamu wa mwili uwe wa kiwango kikubwa, makipa wanahitaji kukimbia mbio fupi, kuruka juu kugeuka kwa haraka sasa kama mwili wa mchezaji haujawa tayari ni rahisi kupata matatizo,” amesema Kigadye ambaye pia alikuwa daktari wa kikosi cha Taifa Stars.

“Wakati huu ambao wachezaji wanatoka kwenye mapumziko ni rahisi kama mchezaji hajajiandaa kupokea mzigo mkubwa wa mazoezi anaweza kuingia kwenye hii shida na kuhusu muda wa kukaa nje inategemea ameumia kwa kiwago gani, unajua maumivu ya goti yamegawanyika kwenye maeneo matatu, Meniscus, Tendol na Ligamenti sasa inategemea na ukubwa wa tatizo alilopata.”


MSIKIE BARKER

Baada ya kuumia kwa Kassali, Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker aliliambia Mwanaspoti kuwa, tukio analiombea lisimfanye kipa huyo kukaa nje kwa muda mrefu huku akisema kitengo cha madaktari wa klabu hiyo wanapambana kumsaidia.

“Naomba sana isiwe ni jeraha la muda mrefu, naomba sana isiwe hivyo, alionekana kuwa na maumivu makali wakati anatoka, ni mmoja ya wachezaji wetu muhimu kwenye kikosi,” amesema Barker.

SIMB 01

“Lakini haina maana kwamba Abel (Hussein) ana tatizo lolote, ana uwezo mzuri na sina tatizo naye.

“Mafanikio ya Simba msimu huu hayawezi kujengwa na wachezaji 11 pekee bali nguvu ya kikosi kizima hasa wakati wa majeraha na adhabu ndiyo maana nasisitiza endapo ikitokea Kassali akakaa nje kwa muda mrefu aliyepo ataendelea na majukumu.”

Alisisitiza alifurahishwa na uwezo alioonyesha Abel baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Kassali alikuwa na utayari na aliisaidia timu.

“Kuhusu muda ambao atakaa nje Kassali ni baada ya tathimini ambayo itafanywa baada ya kurudi Dar es Salaam kutokana na ripoti ya madaktari tutajua kipi tutakifanya kwa muda huo,” amesema Barker.


HALI YA YAKOUB

Hali ya kipa Yakoub Suleiman ambaye alifanyiwa upasuaji wa goti la kulia alipewa muda wa kukaa nje ya uwanja kwa takribani miezi tisa lakini kwa sasa ana miezi minne hivyo imebakia ya kusubiria mitano.

Mtu wa karibu na kipa huyo, amesema: “Ana programu za kufanya mazoezi chini ya daktari Simba ikiwa Dar es Salaam anakuwa anaungana na timu, hali yake inaendelea kuimarika lakini bado atatakiwa kukaa nje kwa muda mrefu.”


WAANDISHI: KHATIMU NAHEKA, OLIPA ASSA NA ELIYA SOLOMON