Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu 64 kuchuana Bodaboda Cup Dar

Dar es Salaam. Ili kuhakikisha sekta ya usafiri wa bodaboda inatambulika vyema kwa jamii, Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam (CMPD) kimeandaa mashindano ya sokayanayolenga kuwakutanisha madereva wote wa bodaboda jijini hapa na kuwaelimisha kuhusu fursa za kiuchumi zilizopo katika sekta hiyo ya bodaboda ikiwemo malipo ya kidijitali, ulinzi na usalama barabarani kama sehemu ya mpango wa kupunguza umasikini.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mashindano hayo yaliyopewa jina Tigo Pesa Mbungi Bodaboda Cup 2023, Juma Kinshashu ambaye ni mwakilishi wa mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema, bodaboda wanapaswa kubadilika na kuwa wa kisasa katika kuzitumia fursa.

CMPD imeandaa mashindano hayo kwa mara ya kwanza ikishirikiana na kampuni ya Tigo, kampuni ya Car & General, EFM, pamoja na Dk Mwaka ForePlan International kuandaa mashindano ya mpira wa miguu yanayofahamika kamaambapo Kishashu alisema;

“Michezo ni afya, michezo ni ajira, ninawapongeza CMPD, serikali inaunga mkono jitahada zozote za michezo, ninawapongeza katika hilo, kupitia Tigo, jambo hili linaenda kuinua hali zenu kiuchumi, sasa mnapaswa kuthamini kazi zenu, mjue mnaenda wapi, lazima muonyeshe kuwa mnabadilika na kuwa wa kiasasa, tujijenge upya”

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo, Mwenyekiti wa Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam, Bwana Michael Massawe amesema; "Sekta ya bodaboda ina fursa nyingi za kiuchumi, hivyo ni muhimu kuwaunganisha na kuwaonyesha jinsi ya kuchangamkia na kunufaika na fursa hizi,"

"Tasnia ya bodaboda inamchango muhimu sana hapa nchini, madereva wengi wa bodaboda ni watu wenye bidii wanaolenga kubadilisha maisha yao, zaidi ya hayo, tasnia yetu ina fursa nyingi za kiuchumi, hivyo bodaboda hawezi kukosa rasilimali za kuboresha maisha yake," aliongeza Massawe

Ofisa Mkuu wa Tigo Pesa Angelica Pesha amesema kupitia amshindano haya madereva pikipiki watapata fursa ya kujifunza njia mpaya ya malipo kwa ajili ya kuongeza kipato cha.

"Tigo tumeona ni vyema kutumia nafasi hii ya kuwakutanisha bodaboda kwa ajili ya kuwapa fursa za kiuchumi ambapo tigo tutakuwa na nafasi ya kuwasaidia madereva pikipiki kutambua namna mpya ya kufanya malipo kupitia “Lipa kwa Simu” ambapo wateja wanaweza kulipa kwa simu zao za mkononi ili bodaboda waweze kupata pesa kupitia njia ya kidijitali” alisema Pesha

Meneja wa Malipo ya Wafanyabiashara wa Tigo Pesa, Edgar Mapande alisema; "Ushirikiano huu na CMPD una manufaa makubwa kiuchumi yatakayo saidia madereva wa bodaboda kutimiza baadhi ya malengo yao, ikiwa ni pamoja na kunufaika na faida za uchumi wa kidijitali kwa kutumia Lipa Kwa Simu ya Tigo Pesa kama suluhisho la kukusanya malipo.

Mashindano ya Tigo Pesa Bodaboda Cup 2023 yatahusisha jumla ya timu 64 kutoka wilaya 5 za Dar es Salaam na semina mbalimbali zitatolewa maeneo ambayo mashindano haya yatafanyikia. Aidha, madereva wa bodaboda watapata fursa ya kujifunza faida za kutumia Lipa Kwa Simu kama njia ya kupokea malipo.

Jumla ya viwanja vinne vya mpira wa miguu vitatumika kwa mashindano hayo, ikiwa ni pamoja na uwanja wa Machava Kigamboni, Uhuru wa Temeke, Ukombozi wa Ubungo na Airwing wa Ilala.

CMPD ni chama kinachosimamia madereva na wamiliki wa pikipiki katika Mkoa wa Dar es Salaam, kilianzishwa mwaka 2016, kinasaidia madereva wa bodaboda kupata mikopo ya pikipiki, viwanja, simu, leseni za udereva pamoja na bima ya afya kupitia taasisi za kifedha nchini.