Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Depu njia panda Yanga


WAKATI mambo yakiendelea kunoga Yanga, hatma ya mshambuliaji, Laurindo Aurelio ‘Depu’ haijajulika kwani kuna uwezekano wa kupewa mkono wa kwaheri wa moja kwa moja au kwa mkopo.


Depu alitua Jangwani Januari 2026 na kupewa mkataba wa miaka miwil, akitokea Radomiak Radom ya Poland. Awali alionekana kuwa mwarobaini eneo la ushambuliaji ambapo alimaliza msimu wa 2025-2026 akifunga mabao tisa Ligi Kuu Bara nyuma ya Prince Dube (10) na kinara wa kikosi hicho, Allan Okello (14).

Chanzo kutoka Yanga kinabainisha kwamba, hivi sasa kuna mazungumzo yanayoendelea kuhusu Depu baada ya eneo la ushambuliaji kuonekana kuwa na idadi kubwa ya wachezaji kufuatia usajili uliofanywa.

Hata hivyo, chanzo kimefichua Yanga imebakiwa na nafasi moja ya kusajili mchezaji wa kimataifa huku viongozi wakisisitiza kuna vyuma viwili vya kimataifa vinashushwa. Ili kufanikisha hilo, mmoja lazima apishe.

Kati ya nyota wawili wanaotajwa kuingizwa kwenye usajili wa wachezaji wa kimataifa ni kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Stephane Aziz KI. Mwingine ni kiungo mkabaji ambaye bado hajawekwa wazi.

Kurejea kwa Aziz KI ndani ya Yanga, Mwanaspoti liliripoti awali ikielezwa kwamba haukutokana na familia aliyoanzisha na mwanamitindo Hamisa Mobetto, lakini mazungumzo na klabu hiyo ambapo pande mbili zilikubaliana kumnunua kutoka Al-Ittihad ya Libya.

Taarifa za ndani zililiambia Mwanaspoti kuwa, dili la kiungo huyo raia wa Burkina Faso liko kwenye hatua nzuri, kwani bosi kubwa wa klabu hiyo amekubali kutoa pesa.

“Stephanie Aziz KI dili lake la kurejea Yanga lipo hatua za mwisho kukamilika baada ya GSM kukubali kulipa Dola 400,000 ili avunje mkataba wake, Yanga iko kwenye hesabu zao wanataka akitoka mtu anaingia mtu na kwa Aziz Ki maana yake akikosekana Okello basi Aziz anaingia.”

Huenda kinachowapa jeuri Yanga ni uwepo wa mastaa wengi hasa eneo hilo la mbele, ukiachana na Depu ambaye anaweza asiwepo msimu ujao, kuna Msenegali mwenye uraia wa Ufaransa, Cheikh Toure, imemuongeza Peter Shalulile kutoka Namibia, huku mshambuliaji mzawa Clement Mzize naye akianza mazoezi akitarajiwa kuwa fiti moja kwa moja Desemba mwaka huu baada ya kupona goti lake, akitangulia kufanyiwa upasuaji. Pia kuna kinda Hussein Mihambo ambaye amesajiliwa na timu hiyo dirisha hili akitokea Mashujaa ya Kigoma.

Kwa upana wa kikosi hicho hasa eneo la ushambuliaji, kunazidi kumpa nafasi ndogo Depu kusalia ndani ya kikosi hicho, kwani mastaa walioshuka wanatarajiwa kufanya makubwa kama inavyotarajiwa kwa upande wake pia.

Ikumbukwe kuwa, Aziz ambaye aliuzwa na Yanga kwenda Wydad msimu uliopita, ambapo huko alicheza miezi nane pekee akiacha rekodi ya kufunga bao moja, huku Yanga akiwa akichafua sana kwa kufunga mabao 39 ndani misimu mitatu, akichukua tuzo ya mfungaji bora katika mwaka wake wa pili Jangwani.

Hesabu za Yanga ziko hivi; wakati Okello ambaye ametua dirisha dogo 2026 na kufunga mabao 14 Ligi Kuu, Aziz yuko nje anapasha ili kuingia kumsaiidia kwani wote ni viungo, wakati ambao Pacome Zouzoua akiwa nje kutokana na majeraha.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema: “Yanga imebakiza kusajili wachezaji wawili wakigeni, hivyo bado watu wanaendelea kuongezwa na kupunguzwa, lakini pia Pacome ameondolewa kwenye mfumo mpaka atakaporudi kwenye hali yake na tumempa muda mpaka dirisha dogo.”

Depu ni miongoni mwa wachezaji 11 wa kigeni waliopo Yanga hadi sasa, wengine ni Cheikh Ibrahima Touré, Albert Kangwanda, Housseine Zakouani, Peter Shalulile, Djigui Diarra, Kouassi Attohoula Yao, Chadrack Boka, Duke Abuya, Maxi Mpia Nzengeli na Allan Okello. Kanuni zinaruhusu timu moja kuwa na nyota 12 wa kigeni, hivyo Yanga kwa kusema imebakisha nafasi mbili, maana yake mmoja anachomoka.