Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF yafafanua ishu ya wachezaji wa Yanga Stars kuondoka

YANGA Pict
YANGA Pict

Muktasari:

  • Katibu Mkuu wa TFF Evance Mgeusa amesema mbali na Yanga klabu zingine zimewasilisha maombi kama hayo na zimeruhusiwa kwa wachezaji wake kurudi kwenye timu zao.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka wazi kwamba sio wachezaji wa Yanga pekee waliopo kwenye kikosi Cha Taifa Stars walioruhusiwa kuondoka kwenye kambi hiyo nchini Morocco.

Katibu Mkuu wa TFF Evance Mgeusa amesema mbali na Yanga klabu zingine zimewasilisha maombi kama hayo na zimeruhusiwa kwa wachezaji wake kurudi kwenye timu zao.

Mgeusa amefafanua kuwa ukiacha Yanga, Simba na Singida nazo zimewasilisha maombi kama hayo ambapo wachezaji wake nao wameruhusiwa kuondoka.

Stars ipo nchini Morocco ikijiandaa kucheza mechi mbili za kirafiki ambapo kesho itajipima na klabu ya AS FAR Rabat kwenye mchezo wa ndani kabla ya Oktoba 5 kucheza dhidi ya wenyeji Morocco ukiwa ni mchezo rasmi wa kalenda ya Mashindano ya Shirikisho la Soka la  Kimataifa (FIFA).
"Sio kwamba ni wachezaji wa Yanga pekee wameruhusiwa kuondoka kwenye kambi ya Taifa Stars, zipo klabu nyingine zimetuma maombi kama hayo na  tumewaruhusu hao wachezaji,"amesema Mgeusa.

"Hao wachezaji bado hawajaondoka, tumekubaliana watacheza mchezo wa kesho na baada ya hapo wataondoka, klabu zingine ni Simba na Singida nazo zimetuma maombi kama hayo na tumewaruhusu.

Aidha Mgeusa ameongeza kuwa  uamuzi wa kuwaruhusu wachezaji hao uliwahusisha benchi la ufundi la Stars chini ya kocha Miguel Gamondi ambaye naye alitoa baraka zake.

"Hizo taarifa za kwamba kocha amechukizwa sijajua zinatoka wapi kwani kabla ya uamuzi huo tuliwahusisha makocha nao wakatoa baraka zao kwenye hili.

"Bado kocha (Gamondi) ana wachezaji wa kutosha kwenye kikosi chake na ratiba zingine zitaendelea kama ambavyo zilikuwa zimepangwa kabla."
Simba na Yanga zinajiandaa na mchezo wa Dabi utakaopigwa Oktoba 10,2026.