Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tembo Queens yatangaza kikosi kuelekea mashindano ya Afrika

TEMBO Pict

Muktasari:

  • Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, chini ya ushirikiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF), yalijikita katika kuwajenga wachezaji kwenye mifumo ya kanuni, utaratibu wa mchezo, pamoja na mbinu za kiufundi kama kupasia na kupiga mashuti.

BAADA ya kukamilika kwa kambi ya mafunzo ya siku 14 iliyokuwa na lengo la kuwajenga na kuwanoa wachezaji wa mpira wa miguu wa wanawake wenye ulemavu, timu ya taifa ya wanawake ya mchezo huo, Tembo Queens, imetangaza kikosi cha nyota 13 watakaowakilisha kwenye mashindano ya Afrika.

Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, chini ya ushirikiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF), yalijikita katika kuwajenga wachezaji kwenye mifumo ya kanuni, utaratibu wa mchezo, pamoja na mbinu za kiufundi kama kupasia na kupiga mashuti.

Akizungumza na Mwanaspoti Kocha Abdul Ally Machine aliyeendesha kambi hiyo alieleza kuwa haikuwa kazi rahisi kupata wachezaji kutokana na changamoto za kijamii.

“Tumepata tabu sana kupata wachezaji wa kike kwa sababu bado jamii haiamini kuwa watu wenye ulemavu wanaweza kucheza mpira na wana haki ya kushiriki michezo. Hata hivyo, tumewaandaa na kuwatengeneza vyema, na sasa Kocha Mkuu pamoja na benchi la ufundi walioteua kikosi rasmi,” amesema Kocha Machine.

“Tayari tumemaliza programu hiyo na tumeionyesha Serikali namna timu iko tayari kushindana na kuiwakilisha nchi vyema.”

Mashindano hayo ya Afrika ya Watu Wenye Ulemavu yanatarajiwa kufanyika nchini Angola Desemba 12, 2026. Awali, Tanzania iliomba kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, lakini iliarifiwa kuwa haiwezekani kwa sasa kutokana na maandalizi yanayoendelea ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Kikosi kilichoitwa chini ya kocha Steven Namwambo, makipa, Priscah Sanga (Njombe), Neema Charles (Dar es Salaam), Mabeki Mayrose Rafael (Dar es Salaam), Benedita Ditivit (Dar es Salaam), Winfrida Benjamin (Morogoro), Maria Chaula (Pwani).

Viungo ni Halima Sanga (Njombe), Neema Lawrence (Arusha)

Shani Mshamu (Dar es Salaam), Amina Frankiwero (Songwe), washambuliaji,  Batuli Alfani (Pwani), Monica Joseph (Pwani) na Wema Yusuf (Dar es Salaam).