Tanzania yatwaa ubingwa CECAFA
Muktasari:
- Mashindano hayo yanashirikisha vijana wenye umri chini ya umri wa miaka 15.Timu ya Tanzania ya Wanawake ya Tanzania chini ya umri wa miaka 15, imefuzu mashindano ya CAF African Schools Football Championship baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kenya katika mechi ya fainali jana.
TANZANIA imeng’aa katika mashindano ya kanda ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ya kuwania kufuzu mashindano ya CAF African Schools Football Chamiponship (ASFC) yaliyofikia tamati jana nchini Rwanda.
Mashindano hayo yanashirikisha vijana wenye umri chini ya umri wa miaka 15.Timu ya Tanzania ya Wanawake ya Tanzania chini ya umri wa miaka 15, imefuzu mashindano ya CAF African Schools Football Championship baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kenya katika mechi ya fainali jana.
Matokeo hayo pia yameihakikishia Tanzania ubingwa wa mashindano hayo ya kufuzu kwa kupitia kanda ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Katika mechi hiyo, mabao ya Tanzania yalifungwa na Salah Msagala, Eva Maiope na Anna Pascal.
Ushindi huo pia uliihakikishia Tanzania zawadi ya fedha kiasi cha Dola 100,000 (Sh265 milioni).
Kenya ambayo imemaliza katika nafasi ya pili, imeondoka na kifuta jasho cha Dola 75,000 (Sh199 milioni).
Ikumbukwe katika mashindano ya Afrika, timu ya Tanzania ya Wanawake wa umri huo imewahi kutwaa ubingwa mara moja.
Wakati huohuo timu ya wanaume umri chini ya miaka 15, imefanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sudan Kusini.
Mabao hayo yamefungwa na Seleman Seleman na France Mkinga.
Kwa kumaliza katika nafasi ya tatu, vijana hao wa kiume wa Tanzania wanaondoka na kitita cha Dola 50,000 (Sh132 milioni).