Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yaporomoka viwango FIFA, Rwanda yapaa

Baadhi wa wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Baada ya chati ya mwezi Oktoba, 2026, Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) litatoa viwango vipya Novemba 18, 2026.

Tanzania imeanguka kwa nafasi tatu katika chati ya viwango vya ubora wa soka ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa mwezi Oktoba 2026.

Katika chati iliyotolewa jana Oktoba 7, 2026, Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya 112 hadi nafasi ya 115 mtawalia.

Kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Guinea Bissau na kiaha kutoka sare ya bao 1-1 na Madagascar katika mechi za kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, kunaonekana kuchangia kuiangusha Tanzania katika viwango hivyo vya ubora wa soka duniani.

Mafanikio ya Rwanda katika mechi mbili za kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Cape Verde na Liberia yameonekana kuwabeba baada ya kupaa kwa nafasi tisa kwenye chati ya viwango vya ubora iliyotolewa.

Rwanda imepanda hadi nafasi ya 119 kutoka nafasi ya 128 ambayo ilikuwepo awali.

Uganda imepanda kwa nafasi mbili kutoka ya 89 hadi ya 87 huku Kenya ikianguka kwa nafasi tano kutoka ile ya 109 iliyokuwepo mwanzo hadi nafasi ya 114.

Burundi imepanda kutoka nafasi ya 142 hadi nafasi ya 140 wakati Ethiopia iliyokuwa katika nafasi ya 143 imeshuka hadi nafasi ya 147.

Hakujawa na mabadiliko katika nafasi nne za juu katika chati hiyo ya viwango vya ubora wa soka duniani.

Hispania imeendelea kuongoza ikifuatiwa na Argentina kisha Ufaransa na England.

Mabadiliko yapo katika nafasi ya tano ambayo sasa inashikiliwa na Ureno ambayo imepanda kwa nafasi moja ikiishusha Brazil iliyokuwa hapo hadi nafasi ya sita.

Viwango vipya vya ubora wa soka duniani vitatangazwa tena Novemba 18 mwaka huu.