Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Twiga Stars yaifuata Botswana kukiwasha Oktoba 9

Muktasari:

  • Twiga Stars imeondoka jana asubuhi ikiwa na jukumu la kuhakikisha inapata matokeo mazuri kwenye Uwanja wa Taifa wa Gaborone kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Oktoba 13 jijini Dar es Salaam.

TIMU ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, imeelekea Gaborone, Botswana, kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa kufuzu Michezo ya Olimpiki 2028 dhidi ya wenyeji Botswana, utakaopigwa kesho Ijumaa, Oktoba 9, 2026.

Twiga Stars imeondoka jana asubuhi ikiwa na jukumu la kuhakikisha inapata matokeo mazuri kwenye Uwanja wa Taifa wa Gaborone kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Oktoba 13 jijini Dar es Salaam.

Kikosi hicho kinachoongozwa na nahodha Opah Clement kitaingia kwenye mchezo huo kikilenga kujiweka kwenye nafasi nzuri kabla ya kurejea nyumbani kumalizia kazi.

Kocha mkuu Bakari Shime amesema maandalizi ya timu yamefanyika kwa muda mfupi kutokana na mabadiliko ya utaratibu wa kuweka kambi, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo wachezaji walikaa pamoja kwa muda mrefu.

Shime alisema mazoezi rasmi yalianza Oktoba 5, ambapo timu ilifanya vipindi viwili siku ya kwanza na kipindi kimoja siku iliyofuata kabla ya kuanza safari.

“Zamani wachezaji walikaa kambini kwa muda mrefu na kupata nafasi ya kuelewana, lakini kutokana na mahitaji ya timu zao, sasa tunakaa muda mchache. Hata hivyo, tunaenda Botswana tukiwa na dhamira ya kufanya vizuri,” alisema Shime.

Twiga Stars inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu mbaya dhidi ya Botswana.

Katika mchujo wa Olimpiki wa mwaka 2019, Botswana iliifunga Tanzania bao 1-0 Gaborone, kabla ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 Dar es Salaam, matokeo yaliyoifanya Botswana kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2.

Hata hivyo, Twiga Stars ililipiza kisasi katika Kombe la Wanawake la COSAFA 2021, ilipoichapa Botswana mabao 2-0 kupitia Donisia Minja na Mwanahamisi Omary’Gaucho’.

Timu hizo pia zilitoka sare ya 0-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Rabat, Morocco, Julai 2022.

Twiga Stars sasa inataka kutumia ubora wa safu yake ya ushambuliaji kupata matokeo mazuri ugenini kabla ya kurejea Dar es Salaam kwa mchezo wa marudiano.