Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania kusaka heshima CECAFA U-20

NGORO Pict

Muktasari:

  • Mchezo wa leo una uzito wake kutokana na mfumo wa mashindano hayo, ambapo Tanzania ipo katika kundi lenye timu tatu pamoja na Rwanda na Ethiopia. Kwenye kundi hilo Rwanda imekusanya pointi moja iliyoipata dhidi ya Ethiopia baada ya dakika 90 kutamatika kwa suluhu.

LEO saa 2:00 Usiku kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Timu ya Taifa ya Tanzanzia chini ya miaka 20 itakuwa na kibarua cha dakika 90 za kuamua hatma ya kwenda hatua ya nusu fainali itakapokabiliana na Ethiopia katika mechi ya pili ya kundi A ya michuano ya CECAFA.

Baada ya kuanza kampeni kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Rwanda Septemba 15, Ngorongoro Heroes sasa inahitaji ushindi mbele ya Ethiopia ili kujisogeza karibu na hatua ya nusu fainali.

Mchezo wa leo una uzito wake kutokana na mfumo wa mashindano hayo, ambapo Tanzania ipo katika kundi lenye timu tatu pamoja na Rwanda na Ethiopia. Kwenye kundi hilo Rwanda imekusanya pointi moja iliyoipata dhidi ya Ethiopia baada ya dakika 90 kutamatika kwa suluhu.

Nahodha wa Ngorongoro Heroes, Arafat Ally, amesema kikosi hicho kinafahamu ukubwa wa kazi iliyopo mbele yao na hakuna mchezaji anayetarajia kupata mchezo mwepesi dhidi ya Ethiopia.

MSU 01

Ameongeza kuwa kila mchezaji amejitayarisha kwa ajili ya mchezo huo na wamejua mapema kwamba wanaweza kukutana na mpinzani wa aina yoyote, hivyo kinachotakiwa ni kuingia uwanjani kwa umakini na kutekeleza majukumu yao.

“Tunafahamu ugumu wa mchezo huu, lakini kila mchezaji amejitayarisha tunawaheshimu wapinzani wetu na tuko tayari kwa yeyote atakayekuja mbele yetu kazi yetu ni kupambana kwa dakika zote na kuhakikisha tunapata matokeo tunayoyahitaji,” amesema Arafat.

Tanzania iliingia kwenye mashindano hayo kwa kujiamini baada ya kuifunga Rwanda mabao 3-0, matokeo yaliyoweka mazingira mazuri kwa vijana hao kabla ya mchezo wa leo.

MSU 02

Mbali na pambano la Tanzania na Ethiopia, leo kutakuwa na michezo mingine miwili kwenye michuano hiyo.

Djibouti itakutana na Sudan saa 10:00 jioni, kabla ya Burundi kukabiliana na Kenya katika mchezo mwingine wa siku hiyo.