Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msudan aigusa Ngorongoro Heroes CECAFA U-20

MSUDAN Pict

Muktasari:

  • Kikosi hicho kilianza kampeni yake kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Djibouti ambayo imeondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kupoteza mechi mbili za kundi B.

KOCHA Mkuu wa Sudan U-20, Mohamed Mousa amesema hadi sasa timu za Tanzania, Rwanda na Uganda ni miongoni mwa timu alizoona zikicheza soka safi katika michuano ya CECAFA U-20 inayoendelea Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kikosi hicho kilianza kampeni yake kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Djibouti ambayo imeondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kupoteza mechi mbili za kundi B.

Akizungumza baada ya mchezo, Mousa amesema kiwango kilichoonyeshwa na timu hizo kinaonyesha ushindani uliopo kwenye mashindano hayo, huku akisisitiza kuwa kila mchezo una changamoto zake na timu yake imekuwa ikijifunza kadri michuano inavyoendelea.

MSU 01

“Tumekuwa tukiona timu nzuri kwenye mashindano haya. Tanzania, Rwanda na Uganda ni baadhi ya timu ambazo nimeziona zikicheza mpira mzuri ushindani ni mkubwa na kila mchezo unahitaji maandalizi,” amesema Mousa.

Sudan sasa inajiandaa kumaliza hatua ya makundi kwa kukutana na Uganda katika mchezo ambao kocha huyo ameuona kuwa muhimu kwa safari yao ya mashindano.

Mousa amesema mchezo huo hautakuwa mwepesi kutokana na ubora wa Uganda, lakini amesisitiza kuwa kikosi chake kiko tayari kupambana kutafuta matokeo yatakayowaweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

MSU 02

“Tunajua Uganda ni timu nzuri na mchezo huu utakuwa mgumu, lakini tuko tayari. Tunahitaji pointi tatu na tutapambana kuhakikisha tunazipata ili kuendelea na safari yetu katika mashindano,” amesema.

Kama Sudan itashinda mchezo huo itakuwa na nafasi ya kufuzu hatua ya nusu fainali kwakuwa itakuwa imefikisha pointi sita.