Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tambwe: Singida Black Stars tunataka robo CAF

TAMBWE Pict

Muktasari:

  • Tambwe, ambaye aliwahi kufanya makubwa akiwa mchezaji wa Simba na Yanga, ikiwemo kutwaa tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara, amesema mafanikio ya msimu uliopita yamewapa nguvu ya kuongeza kiwango cha malengo yao msimu huu.

MENEJA wa Singida Black Stars, Amissi Tambwe, amesema msimu huu wana kiu kubwa zaidi baada ya kuvuka malengo yao msimu uliopita, akifichua safari yao mpya ya kimataifa imeelekezwa moja kwa moja kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.

Tambwe, ambaye aliwahi kufanya makubwa akiwa mchezaji wa Simba na Yanga, ikiwemo kutwaa tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara, amesema mafanikio ya msimu uliopita yamewapa nguvu ya kuongeza kiwango cha malengo yao msimu huu.

Singida Black Stars msimu uliopita ilimaliza ndani ya nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC na pia kufika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, jambo ambalo sasa limewafanya viongozi wa klabu hiyo kuweka mipango mikubwa zaidi.

SINGI 01

“Tuliweka malengo msimu uliopita ya kumaliza ndani ya nafasi nne za mwanzo na tukafanikiwa. Kwenye CAF tulijiwekea lengo la kufika hatua ya makundi na tukafika kwa hiyo msimu huu tumejiwekea malengo ya kufika robo fainali kwenye michuano ya CAF na inawezekana. Hayo ndiyo malengo yetu,”  amesema.

Kwa upande wa Ligi Kuu, Tambwe amesema hawataki kuridhika na nafasi ya nne waliyofikia msimu uliopita, badala yake wanataka kusogea zaidi na kuingia katika ushindani mkubwa wa nafasi za juu.

“Msako wetu msimu huu ni kupanda tena. Msimu uliopita tulijiwekea lengo la kuwa kwenye nne bora ili tushiriki mashindano ya kimataifa, lakini msimu huu tunataka kupanda zaidi,” amesema.

SINGI 02

Tambwe anaamini hilo linawezekana kutokana na mabadiliko yaliyofanyika ndani ya timu, kuanzia usajili hadi maandalizi ya kikosi huku wakiamini wana uwezo wa kupambana na timu kubwa zaidi.

“Vitu vingi vimebadilika, kwa hiyo tunaamini msimu huu tutafanya vizuri zaidi. Tunataka kusogea mbele na tunaamini inawezekana,” amesema.

Singida BS imefuzu hatua ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitoa Al Ghazala ya Sudan Kusini kwa jumla ya mabao 10-1, sasa inakutana na Tusker ya Kenya kuwania kufuzu makundi.