Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kassano aondoka Singida BS, Kidawawa amrithi

CEO Pict

Muktasari:

  • Katika taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo leo Septemba 13, 2026, uongozi wa klabu hiyo umesema umepokea barua ya Kassano akiomba kujiuzulu na umeamua kukubaliana na ombi hilo.

SINGIDA Black Stars imeanza ukurasa mpya wa uongozi baada ya Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Kassano Jonathan, kuwasilisha ombi la kujiuzulu nafasi yake, huku Tabitha Kidawawa akichukua nafasi yake.

Katika taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo leo Septemba 13, 2026, uongozi wa klabu hiyo umesema umepokea barua ya Kassano akiomba kujiuzulu na umeamua kukubaliana na ombi hilo.

“Uongozi unamshukuru sana ndugu Kassano Jonathan kwa mchango wake mkubwa katika Klabu tangu achukue nafasi hiyo. Uongozi unamtakia kila la heri katika hatua yake nyingine na kumhakikishia kuwa Singida BS kutabakia kuwa nyumbani kwake,” imeeleza taarifa hiyo.

Kassano amekuwa sehemu ya uongozi wa Singida Black Stars katika kipindi ambacho klabu hiyo imeendelea kujijenga na kuwa moja ya timu zinazoshindana katika soka la Tanzania.

Kiongozi huyo alikuwa Mtendaji Mkuu wa Singida Black Stars tangu mwaka 2024, ambapo kuondoka kwake sasa kunafungua ukurasa mpya kwa klabu hiyo.

Kabla ya uteuzi, Kidawawa alikuwa akifanya kazi kama Mkurugenzi wa Masoko na Mashindano wa Singida Black Stars, nafasi aliyopewa Februari 2026.

Uzoefu huo ndani ya klabu sasa umemuweka katika nafasi ya juu zaidi ya uongozi, akiteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu na kusaidiwa na Naibu wake, Muhibu Kanu.